WAJASIRIAMALI WADOGO 283 IRAMBA WAELIMISHWA UBUNIFU, MASOKO NA USAJILI KUPITIA MFUMO WA WAJASILIAMALI PORTAL (WBN-MIS)
Wajasiliamali wadogo 283 Wilayani Iramba wameshiriki kongamano la siku moja lililolenga kuwajengea uwezo katika nyanja za ubunifu, mitaji, na masoko.
Kongamano hilo lilifanyika tarehe 2 Agosti 2025 katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba chini ya uratibu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum, ambao huhusika kuwatambua na kuwasajili wajasiriamali wadogo kupitia mfumo wa kidigitali wa Wajasiliamali Portal (WBN-MIS).
Katika kongamano hilo, washiriki walipatiwa elimu juu ya fursa za masoko, mbinu za ubunifu katika biashara, upatikanaji wa mitaji, pamoja na umuhimu wa kujisajili katika mfumo wa WBN-MIS ili kutambulika rasmi na kupata vitambulisho.
Akitoa wasilisho, Afisa Maendeleo ya Jamii, Mtaki Samsoni Magina, alisisitiza umuhimu wa kuelewa matumizi ya mfumo huo, vitu muhimu vya kuzingatia ili kupata kitambulisho, faida za kuwa na kitambulisho, pamoja na fursa za mitaji na masoko kwa wajasiriamali wadogo.
Kongamano hilo ni hatua muhimu katika kuinua sekta ya ujasiriamali wilayani Iramba, likiwaunganisha wajasiriamali wadogo na mifumo rasmi ya kibiashara.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.