Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wamefanya ziara ya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa Wilayani Iramba
Ziara hiyo ni utaratibu wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri kwa kila robo Mwaka, ambapo ukaguzi huu ni wa robo ya kwanza Kipindi cha Mwezi Julai- Septemba 2023 kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.
Ukaguzi huo umehusisha Wataalam mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ambapo kwa pamoja wamekagua Mradi huo unaojengwa kwa mfumo wa "Force Account" Ujenzi wa nyumba ya Watumishi 2 in 1 Shule ya Sekondari Ndulungu,Ujenzi wa nyumba ya Watumishi 2 in 1 Shule ya Msingi Makungu,Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Iramba,Ujenzi wa chumba kimoja cha darasa Shule ya Msingi Kinakumi,Ujenzi wa matundu ya Vyoo na Tangi la kununia maji Zahanati ya Usure
Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Iramba kupitia mradi wa SEQUIP ni moja kati ya utekelezaji miradi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya RAIS TAMISEMI.
" Kwa sasa majengo yanayojengwa katika Shule mpya ya Sekondari Iramba iliyopo Old Kiomboi ni Jengo la Utawala, Madarasa,Chumba Cha Kompyuta,maabara
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mhe. Philip Manguli na Wajumbe wa Kamati ya Fedha kwa niaba ya Baraza la Halmashauri wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa ya ujenzi wa miradi mingi ya maendeleo katika Halmashauri ya Iramba
Hata hivyo, Mhe. Justus Makala Mjumbe wa Kamati hiyo ametoa angalizo kuwa, Kamati za ujenzi ziongeze umakini katika kusimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Iramba ikiwa ni pamoja na kuweka nyaraka zote za mradi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.