WAKULIMA WILAYANI IRAMBA MKOANI SINGIDA WAAGIZWA KUTUNZA CHAKULA
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda,Amewaagiza wakulima Wilayani humo,Kuhakikisha wanahifadhi Chakula isije ikatokea kuuza chakula chote na ikafika masika,hakuna
Chakula.
Hayo yamejiri wakati wa ziara yake ya Kukagua miradi ya Maendeleo na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua baadhi ya changamoto zinazowezekana chini yake.
Mwenda amepiga marufuku wafanyabiashara wote wa mazao wa ndani na nje ya nchi kufika ofisini kwake na kuongea nao juu ya utaratibu wa kununua mazao ndani ya Wilaya ya Iramba.
"Nimemwagiza Afisa uhamiaji Wilaya kuwaita wanunuzi wa Mazao wa kutoka Nje ya Nchi wafike ofisini kwangu na niongee nao niwape utaratibu wa kununua mazao,Vinginevyo hakuna mtu wa kununua mazao hapa waende kokote lakini siyo Iramba" Amesema Mwenda.
Aidha DC Mwenda,Amesema hataki kuona mnunuzi yoyote yule ananunua mazao mashambani kwa wakulima na badala yake wanunulie sokoni, kwenye bei ya Jumla na siyo kufika mashambani au nyumbani kwa wakulima na kuwanyonya wakulima kwa bei ya Chini.
Katika suala la Vipimo,Amewatahadharisha wakulima kutopimiwa mazao yao na Vipimo vya wafanyabiashara kwani ni vikubwa na vinawapunja sana wakulima badala ya kupima kilo 20 wao kipimo Chao ni kilo 22 jambo ambalo amesema halitaki liendee Wilayani kwake
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.