Walimu wa Taaluma 40 kutoka shule za msingi Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wamepatiwa mafunzo ya siku mbili (16-17 Juni 2025) kuhusu mbinu bora za kufanya tathmini na kutoa mrejesho katika ufundishaji na ujifunzaji. Mafunzo hayo yamefadhiliwa kupitia Programu ya Shule Bora kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uingereza.
Mafunzo hayo yalifanyika katika shule ya Msingi Kiomboi Bomani, yakiongozwa na mwezeshaji Bi. Happiness Mposindawa na yalilenga kuwajengea uwezo walimu wa taaluma katika kufanya Tathmini na kutoa mrejesho katika mchakato mzima wa ufundishaji na Ujifunzaji.
Pia, yameangazia mbinu za tathmini endelevu, matumizi ya vigezo sahihi vya upimaji, na njia shirikishi zinazomwezesha mwalimu kumtambua kwa usahihi mwanafunzi anapopitia mchakato wa kujifunza. Kupitia mafunzo hayo tathmini inatumika kama chombo cha kujenga, siyo tu kupima maarifa.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.