Akizungumza Disemba 19, 2024 katika ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri Afisa Elimu Wilaya, Idara ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwalimu Rose Willgeofrey Kibakaya amewataka Walimu Kuzingatia mafunzo hayo ili kuinua taaluma na kuwawezesha wanafunzi wa awali kufahamu kusoma, kuhesabu na kuandika.
"Nia ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kubadilika tutoke hapa tulipo, Kwahiyo tuna Imani mtafundishwa vizuri na mtakuwa ni chachu kwa maendeleo ya Elimu Wilaya ya Iramba.Tunawategemea sana naomba mafunzo hayo myasikilize vizuri." Alisema Mwalimu Rose Kibakaya
Kwa upande wake Afisa Tawala kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) idara ya Usimamizi wa Elimu Joyce Henry kitundu amesema zoezi hili ni kwaajili ya kuwawezesha Walimu wa awali kufahamu mitaala iliyoboreshwa ili kuitumia vyema katika ufundishaji.
"Tunataka Madara ya Elimu ya awali yaongee ili mtu alifika shule akutane na darasa lenye picha na vitendea kazi ili apende na kuhamasika kwenda kujifunza. Kwahiyo zile zana watakazozitengeneza Walimu zitawasaidia watoto namna ya kujifunza Elimu yao ya awali kabla ya Elimu ya Msingi." Alisema Joyce Henry
Mafunzo hayo yalianza Disemba 16-18, 2024 kwa Walimu Mahiri pamoja na mthibiti Ubora wa shule kwa ngazi ya Wilaya, na kuendelea kwa siku nne kwa Walimu wa awali na siku tatu kwa Walimu wakuu na na walimu wanaofundisha darasa la Awali yatahitimishwa Jumamosi Disemba 22, 2024.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.