Walimu Wakuu 108 wa Shule za Msingi na Maafisa Elimu kata 20 Wilayani Iramba wapewa Mafunzo Endelevu ya Usimamizi wa Ufundishaji na Ujifunzaji fanisi kupitia Jumuiya za kujifunza za Walimu Wakuu na maafisa Elimu Kata.
Mafunzo hayo ya Siku tatu yanayo ratibiwa na Mradi wa Serikali wa Shule Bora yameanza Machi 19-21, 2025 katika Shule ya Msingi Kiomboi Bomani.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl. Rose Willgeofrey Kibakaya amewasisitiza Walimu Wakuu na maafisa Elimu Kata kuendelea kuwa na ushirikiano mahali pa kazi huku akitoka wito kwao kuyatumia mafunzo hayo kuongeza ufaulu wa Madarasa yote ya Mtihani.
"Nia ya Shule Bora ni kuwapa uwezo viongozi na ninyi ni viongozi, uwezo huu ni kupitia Mawasiliano mahali pa kazi. Jumuiya inayojifunza lazima itambue kuwa mahali pa kazi panahitaji ushirikiano. Pia Nia ya mafunzo haya ni kuongeza ufaulu kwa Madara ya Mtihani ndio maana leo mnapata mafunzo ya jinsi gani kuwa na mawasiliano na ushirikiano ndani ya Jumuiya ya Ujifunzaji". Amesema Mwalimu Kibakaya.
Kwa upende wake Mwezeshaji Kitaifa Zipora John Hosea amesema Mradi wa Shule Bora unasimiamia nyanja kuu nne ambazo ni ushirikishwaji wa Jamii katika masuala ya kielimu, masuala ya ujumuishi, Uongozi na Utawala, Ufundishaji na Ujifunzaji na umelenga kuhakikisha mikoa legwa inafanya vizuri katika masuala ya kitaaluma na sekta ya Elimu kwa ujumla.
"Shule Bora inasimamia sana kuhakikisha mikoa hii Tisa ukiwemo mkoa huu wa Singida inafanya vizuri katika masuala ya Kitaaluma na sekta ya Elimu. Tupo hapa kuwasaidia viongozi hawa kuona wanawezaje tatua changamoto za Kiuongozi na kushirikishana katika kuinua maeneo yao kitaaluma." Amesema Bi Zipora Hosea.
SHULE BORA ni mradi wa Serikali ufadhiliwa wa Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK aid kwa lengo la kukuza na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji ndani ya shule ili kuboresha Elimu katika mikoa Tisa nchini mambayo imekuwa haifanyi vizuri kitaaluma. Mikoa hiyo ni pamoja na Singida, Katavi, Rukwa, Dodoma, Mara, Simiyu, Pwani, Tanga na Kigoma.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.