Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni ametoa ahadi mbalimbali kwa wahitimu wa mafunzo ya BONGA na TVET yaliokuwa yakiendeshwa na Shirika la SEMA kata ya Ulemo na Kinampanda.
Ahadi hizo zimetolewa leo Alhamisi Machi 11, 2020 wakati wa mahafali ya wahitimu wa BONGA na TVET katika ukumbi wa Profesa Majule uliopo kata ya Kinampanda Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.
Akiongea na Wahitimu hao, Mwageni amewaambia kuwa kama hawatoyaingiza mafunzo hayo katika utendaji yatakuwa hayana maana huku akiwataka kuunda vikundi ili wapate sifa ya kupata mikipo inayotolewa na Halmashauri hiyo.
“ Niwaombe mtambue kuwa pesa za kuwakopesha tunazo, hivyo watakokamilisha usajili wao kwa wakati watapatiwa mikopo ya mwaka huu,” amesema Mwageni na kuongeza
“ Mtumie fursa ya uwepo wa stendi mpya ya mabasi Misigiri kwenda kuzindua utoaji wa huduma mbalimbali ikewemo chakula kwa wasafiri watakaokua wanapita hapo.”
Mwageni amewaahidi wahitimu waliohitimu mafunzo ya kuchomelea kuwapatia chumba watakachotumia shunghuli zao kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kulipa pesa ya pango eneo la ulemo.
Kwa wale waliohitimu mafunzo ya kilimo na ufugaji, Mwageni amewaahidi kuwapatia mbegu za viazi lishe, mbegu za matunda ya pensheni na Viriba kilo 10 kwa ajili ya kuotesha mipapai ya kisasa na yakienyeji huku akiwataka kutumia fursa hiyo kuwa mawakala wa kuzalisha na kuuza mbegu.
Halikadhalika Mwageni amewaasa wahitimu hao kufanya shughuli za halali ili kupata pato la halali huku akiwaonya kujiingiza kwenye tabia za utapeli kwa lengo la kupata utajiri wa haraka.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la SEMA, Ivo Manyaku amesema kuwa jumla ya wahitimu 295 kutoka katika Wilaya ya Manyoni, Ikungi na Iramba wamehitimu mafunzo hayo.
Manyaku amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imekua yakwanza kwa kuwa na wahitimu 115 ukilinganisha na wale waliohitimu kutoka Wilaya ya Manyoni na Ikungi.
Aidha Mkurugenzi wa SEMA amewaahidi wahitimu hao wakikamalisha uundaji wa vikundi na usajili atawapatia vifaa vya kufanyia kazi.
Naye mmoja wa wahitimu kutoka kata ya ulemo, Monica Zakayo amesema kuwa mafunzo hayo yamewajengea ujasiri wa kujitambua ,kujiamini na kufanya maamuzi sahihi.
Zakayo amesema wameweza kupata ujuzi wa upambaji, uchomeleaji, ususi wa saluni na urembo, upishi, kilimo na ufugaji, ufundi wa pikipiki na ufundi wa umeme, hivyo kuwawezesha kutengeneza sabuni za maji ya mikono, kufulia, sabuni za kuondoa mabaka, kupika vyakula mbalimbali , kupamba kumbi mbalimbali na kilimo cha mbogamboga ambavyo vimewapatia mwanga na matumaini ya maisha.
Kwa upande wake mmoja wa wazazi, Izrael Mkumbo ameushukuru uongozi wa serikali na Shirika la SEMA kwa kukubali mradi huo kufanyika kata ya Ulemo na Kinampanda na kuwataka wahitimu hao kuyafanyia kazi yale yote waliojifunza.
Mradi wa BONGA na TVET ni programu inayoendeshwa na Shirika la SEMA linalowalenga vijana wa kike na kiume (13 – 30) walionje ya mfumo wa elimu ili kuwapatia stadi za maisha kuhusu usafi, baleghe na ujana, haki za wanawake, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia na elimu ya ujasiriamali.
Mafunzo hayo yalianza July mwaka jana na kuhitishwa Mach 2020.
SMWISHO
Mkurugenzi wa Shirika la SEMA akiwaasa wahitimu wa mafunzo ya BONGA na TVET yaliofanyika katika ukumbi wa Profesa Majule Kinampanda Wilayani Iramba. Picha Hemedi Munga
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Gene Ng’ondi akiwaasa wahitimu wa mafunzo ya BONGA na TVET yaliofanyika katika ukumbi wa Profesa Majule Kinampanda Wilayani Iramba. Picha Hemedi Munga
Wahitimu wa mafunzo ya BONGA na TVET waliopata ujuzi wa ususi na urembo wakionesha ujuzi wao wa ususi wa nywele katika mahafali yaliofanyika katika ukumbi wa Profesa Majule Kinampanda Wilayani Iramba. Picha Hemedi Munga
Wahitimu mbalimbali wa mafunzo ya BONGA na TVET wakifuatilia mada mbalimbali za viongozi wakati wa mahafali yaliofanyika katika ukumbi wa Profesa Majule Kinampanda Wilayani Iramba. Picha Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.