Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kufanya usafi na kuzingatia matumizi sahihi ya vyoo Pamoja na kunywa maji safi na salama ili kuepukana na ugonjwa wa Kipindupindu.
Dc Mwenda ameyasema hayo Novemba 5, 2024 katika mikutano wa hadhara na wananchi wa Vijiji vya Kata ya Ndulungu Alipofanya Mikutano ya hadhara kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi kwenye Vijiji vya Kipuma,Ndulungu, Mwanduigembe na Mahola.
“Niwaombe wananchi kuzingatia usafi na kwa mgonjwa yeyote yule ambao ana dalili za ugonjwa huu ikiwa ni kutapika na kuharisha basi awaishwe kwenye kituo cha afya na mtoe taarifa kwa viongozi ili hatua za haraka zichukuliwe kwani kipindupindu kipo ambapo ni Wilaya ya Jirani hivyo lazima tuhakikishe tunachukua tahadhari ya hali ya juu ”. Amesema DC Mwenda.
Aidha Mwenda amesema kila wananchi anawajibu wa kulinda afya yake na familia yake kuwakinga na madhara Pamoja na mlipuko huu wa kipindupindu kwa kutumia maji safi na salama kwa kuyatibu na dawa au kuchemsha na kuhifadhi sehemu iliyo salama.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba Dkt. Glory Andrew amehimiza matumizi sahihi ya vyoo na kuwataka wananchi wote wazingatie usafi wa mazingira ili kuendelea kuudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu usiingie kwenye maeneo yao
Mganga Mkuu amesema ni wajibu wa kila mwananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Kipindupindu na kufuata ushauri wa wataalamu katika kukabiliana na ugonjwa huu.
Hata hivyo amewataka watendaji wa kata,Vijiji kuhakikisha wananchi wote wanatumia vyoo na yule atakaebainika hana choo katika kaya yake awajibishwe kisheria.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.