WANANCHI IRAMBA WANUFAIKA NA HATI MILIKI 1711 KUPITIA MRADI WA UKIJANI UNAOTEKELEZWA NA HELVETAS
Zaidi ya wananchi 1,700 katika Wilaya ya Iramba wamepata hati miliki za kimila kupitia Mradi wa UKIJANI, unaotekelezwa na shirika la Helvetas kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Hafla ya ugawaji wa hati hizi imefanyika Februari 4,2025 Wilayani Iramba, ikihudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo, na wanufaika wa mradi. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mkoani Singida Suleiman Mwenda.
Katika hotuba yake, DC Mwenda amewashukuru waandaaji wa hafla hiyo na kusisitiza umuhimu wa umiliki wa ardhi kwa maendeleo ya wananchi. Alisema hati miliki hizo 1,711, ambazo kati yake 1,077 zinamilikiwa na wanawake, zitachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuimarisha usalama wa ardhi, kuongeza thamani ya umiliki, na kupunguza migogoro ya ardhi.
"Napenda niwapongeze wananchi, mamlaka za vijiji, halmashauri ya wilaya, na wadau wote waliohusika katika mchakato huu. Hii ni hatua kubwa katika kuhakikisha usalama wa milki za ardhi na kuleta maendeleo endelevu," Amesema DC Mwenda.
Mchakato wa Upatikanaji wa Hati Miliki
Mradi wa UKIJANI umetekelezwa katika vijiji vitano vya Mbelekese, Kikonge, Usure, Kinkungu, na Tyeme, vilivyopo katika kata za Mbelekese na Mtoa. Mchakato wa uwezeshaji ulijumuisha hatua tatu kuu:
Kwa upande wake Meneja Mradi wa Ukijani Bi. Shoma Nangale amesema kuwa Ukusanyaji wa Taarifa za Upimaji Maombi ya umiliki wa ardhi yalikusanywa na wataalamu wa upimaji kwa kushirikiana na timu za mipango ya matumizi bora ya ardhi.
Uandaaji wa Hati Miliki– Taarifa zilihakikiwa na hati miliki kuchapishwa kupitia mfumo wa kisasa wa kidigitali, ambapo hekta 2,408.29 za ardhi zilipimwa na kusajiliwa.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.