Kuelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, Wasimamizi wakuu wa vituo vya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wasimamizi wasaidizi pamoja na Makarani waongoza vituo wameapishwa Kiapo cha Utii na Uadilifu leo tarehe 24.11.2024 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Kizaga, kabla ya kupatiwa Semina juu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Wasimamizi hao wamepewa mafunzo yatakayo wawezesha kwenda kusimamia Sheria, Kanuni pamoja na Taratibu zilizowekwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Haya yamefanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27.11.2024 ambapo wananchi wa Iramba watashiriki katika Uchaguzi wa viongozi watakaosimamia Serikali za Vijiji na Vitongoji.
Ikumbukwe kuwa Iramba inatarajia kufanya uchaguzi ambao utatoa viongozi katika Vijiji 70 vyenye vitongoji 393 katika kata zote 20.
Aidha Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Bi. Magreth Christian Segu amewaasa wasimamizi hao pamoja na Makarani kusimamia viapo vyao. Pia amendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza wananchi wa Iramba kujitokeza kwa Wingi kupiga Kura tarehe 27.11.2024 ili kutopoteze haki ya kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo.
"Hakikisheni mnakwenda kuifanya kazi hii kwa Uadilifu mkubwa na kutanguliza maslahi ya nchi, sitegemei kusikia Kuna mtu amefanya kinyume na Miongozo na Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024" Amesema Bi Magreth Segu
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.