WATANZANIA WATAKIWA KUTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUJIFUNZA SHUGHULI ZA UHIFADHI
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amewasihi Watanzania kutembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ili kujifunza shughuli mbalimbali za Uhifadhi na Historia ya maisha ya mwanadamu.
Mwenda amesema hayo Agosti 5, 2025 Nzuguni Jijini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, katika maonesho ya 32 ya wakulima, wafugaji na wavuvi (Nanenane) huku akiipongeza Wizara hiyo kwa kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa watazamaji kufanya Utalii wa ndani kupitia rasilimali za taifa zilizopo hapa nchini.
"Kwakweli ni eneo muhimu kutembelea hasa kwa viongozi hata kwa wananchi, kwa watoto na wakubwa kuna sehemu ya makumbusho ya vitu vya asili inayoonesha mabadiliko ya maisha, kutoka zama zilizopita mpaka sasa, lakini pia watapata fursa ya kujifunza historia ya nchi yetu, haya yote yanapatikana katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii." alisema DC Mwenda.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.