By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba.Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula ameipongeza Timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya za Halmashauri (CHMT) kwa kuvuka lengo katika kampeni ya chanjo ya surua rubella na Polio.
Luhahula ameyasema hayo leo Jumatano Novemba 06, 2019 wakati akipokea taarifa fupi ya tathimini ya kampeni ya chanjo ya surua rubella na polio ukumbi mdogo wa Halmashauri, wilayani Iramba Mkoa wa Singida Tanzania.
Akiwasilisha taarifa fupi ya mafanikio ya uchanjaji wa chanjo ya surua rubella na polio mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mratibu wa Chanjo Wilaya, Jackson Shilla amesema watoto 42,778 wamechanjwa chanjo ya surua rubella huku watoto 23,503 wamechanjwa chanjo ya polio.
Uchanjaji huo umevuka lengo lililokuwa limekusudiwa kuchanja watoto wote wenye umri wa miezi 9 hadi chini ya miaka mitano. Aliongeza Shilla
Akichangia mada katika kikao hicho Afisa Takukuru, Benjamin Maysaga ameitaka Timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya za Halmashauri (CHMT) kutoa elimu ya chanjo hizo kwa wafugaji na wale wanaoendesha zoezi hilo huku akiwatahadharisha kujiepusha na rushwa.
Kampeni ya chanjo ya surua rubella na polio ilifanyika nchi nzima kuanzia Oktoba 17 hadi 21, 2019 chini ya Wizara ya Afya, Ustawi wa jamii, Jinsia Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Afya Dunia (WHO), UNICEF na wadau wengine wa maendeleo.
Chanjo hizo zitaendelea kutolewa chini ya kauli mbiu isemayo “Chanjo ni kinga kwa pamja tuwakinge”
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula akiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya afya ya msingi PHC iliyofanyika leo Novemba 06, 2019 ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.