Na Hemedi Munga
tehama@irambadc.go.tz
Singida - Iramba. Waumini wa dini ya Kiislamu na Kikistro wilayani Iramba mkoa wa Singida wamemuombea dua ya Kheri na mafanikio ya kuliongoza Taifa la Tanzania Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Maombi hayo yamefanyika katika ukumbi mkubwa wa Mikutano ya Halmashauri ya wilaya hiyo katika hafla fupi ya kufuturisha waumini iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya hiyo kwa kushirikiana na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
Akiongea katika hafla hiyo, Shekhe Mkuu wa Msikiti wa Taqwa mjini Kiomboi na Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Amani, Al haji Shekhe Omari Hassan aliwakumbusha waumini hao kuwa Ramadhani ni utakaso kwa kila mwanadamu kujisafisha kuanzia nafsi, mwili, mavazi na matendo yake.
Akinukuu maneno matakatifu toka katika kitabu kitukufu cha qur an, Shekhe Hassan alisema kuwa wanaadamu wamefaradhishiwa kufunga kama vile walivyofaradhishiwa waliokuwa kabla yao.
Aidha, Shekhe Hassan alifafanua kuwa swala la kufunga litakuwa lilianzia toka kwa Mtume Adam (A.S) mpaka kwa Mtume Mohammad (S .W. A), hivyo ndio maana ibada ya funga wanaifunga kwa nguvu kubwa.
Kufuatia Ibada hiyo kuwa katika kumi la mwisho katika Mwezi wa Ramadhani, Shekhe Hassan aliiombea dua Nchii hii iendelee kuwa na amani na salama muda wote.
Aidha, aliwaombea Viongozi wote akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwa na afya njema, msimamo, amani, upendo na makazi mema kwa ajili ya kuitengeneza nchi hii isijeyumba.
“Ewe Mwenyezi Mungu tunakuomba mjalia Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kuwa na ujasiri, umahiri, nguvu na ukakamavu wa hali ya juu na uumuongezee busara, kumzidishia elimu na ufahamu wa kuliongoza Taifa hili kwa uadilifu.” Aliomba al haji Hassan na kuongeza kuwa
“Tukiwa katika kumi la mwisho la Mwezi wa Ramadhani tunaomba dua yetu utukubalie Ewe mwenyezi Mungu!”
Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Kamati ya Amani ya wilaya hiyo mchugaji wa Kanisa la KKKT, Elitegemeo Mpumpa alisema kuwa thamani ya mtu ipo pale mtu anapofunguliwa kutoka kwenye ubinafsi, hivyo alimuomba Mkuu huyo wa wilaya kuendelea na moyo huo wa kuwakutanisha viongozi hao.
Akinukuu maneno matakatifu toka katika kitabu cha Zaburi ya 133 mstari wa kwanza, Mchungaji Mpumpa alisema kuwa Tanzama jinsi ilivyo vyema na kupendeza ndugu wakae pamoja kwa umoja, hivyo katika kikao hichi lipo jambo la kimungu ambapo Mungu amependezwa kuona wao wamekaa pamoja bila ya kujali dini zao.
“Kwa kweli jambo hili ni jema na lakiibanda ambalo linampendeza Mungu, hivyo tunakuomba Mkuu wa Wilaya uendelee na Moyo huo huo.” Alisema
Aidha, alimpongeza na kuahidi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa namna ambavyo anaendelea kuiongoza nchi na maendeleo makubwa anayoyaleta huku akitolea mfano wa barabara ya Ruruma iliyopo Mji mdo wa Kiomboi wilayani hapo ambapo awali barabara hiyo ilikuwa ni makorongo tu lakini sasa imetengenezwa watu wanapita bila shaka kabisa.
Akiongea katika hafla hiyo fupi Mkuu wa Wilaya hiyo, Suleiman Mwenda aliwaasa waumini hao kuwa wao ni watu wa Taifa moja, hivyo wanapaswa kuendelea kuvumiliana na kuishi kwa upendo na kushirikiano kwa amani.
Hata hivyo, Mwenda aliwakumbusha kuwa kusanyiko hilo ni utamaduni wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla kuwa watu wakakaribishana na kula chakula pamoja.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Michael Matomora alitumia hafla hiyo kuwaomba waumini na viongozi wa dini kuwahamasisha waumini na wananchi waliowazunguka kuweka vibao kwa taratibu, vipimo na gharama zilizopo kwa watendaji wa vijiji.
“Nitumie fursa hii kuwaomba Viongozi na waumini kutumia majukwaa yetu kuwahamasisha watu kutekeleza hili na kujiandaa na zoezi la sensa.” Alisema
Aidha. Aliongeza kuwa kukamilika kwa Mfumo wa Anwani za Makazi kutarahisisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
MWISHO
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.