Hemedi Munga, Irambadc
Iramba.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuhadi Dkt Mwigulu Nchemba mbunge wa Iramba Magharibi vituo vingine vya afya kwa ajili ya Tarafa ya Shelui na Tarafa ya Kisiriri.
Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo leo oktoba 6, 2019 katika uwanja wa CCM iramba.
Akiwahutubia wananchi Waziri Mkuu, Majaliwa amesema kuwa serikali ina nia yakuhakikisha hospitali ya kiomboi inakuwa vizuri huku akiitaka halmashauri kukamilisha ujenzi wa zahanati kila kijiji.
Serikali imejenga vituo 352 vya afya nchi nzima ambapo inahitaji vituo hivyo kutoa huduma zote.
Aidha amewaambia wananchi kuwa serikali kila mwezi inaleta pesa za dawa na kuwataka kuwa walinzi wa dawa hizo huku akiwakata madaktari kuacha tabia ya kuwaandikia wagonjwa dawa na kuwaambia wakanunue.
Kwa upande wa elimu, Waziri Mkuu, Majaliwa amesema serikali imetoa maagizo ya kila kijiji kuwa na shule ya msingi huku akiwataka wazazi kupeleka watoto shule.
“ Maafisa Elimu simamieni hili na hakikisheni hakuna michango ya hovyo hovyo” Alisema Waziri Mkuu
Kiasi cha 24bilioni zinatolewa kwa kila mwezi zinazokwenda shuleni kusaidia mambo mbalimbali zikiwemo chaki.
Kwa upande wa sekta ya maji, Waziri Mkuu, Majaliwa amesema tayari wameleta 9.6milioni kwa ajili ya kupeleka maji kwa wananchi.
Upelekaji wa fedha kwa ajili ya maji kwa wananchi ni utekelezaji wa kampeni iliyoanzishwa na Mh, Rais John Pombe Magufuli.
“ Malengo ya serikali kila kijiji kiwe na kisima, tulianza, tunafanya na tunatekeleza” Alisema Waziri Mkuu
Kwa upande wa barabara , Waziri Mkuu , Majaliwa amesema barabara ya mandewa mpaka kizaga ipo hatua ya tatu ya tathimini.
Naye Dkt Mwigulu Nchemba Mbunge wa Iramba Magharibi amemuomba Waziri Mkuu, Majaliwa ujenzi wa madaraja makubwa.
“Kutokana na jeografia ya wilaya ya Iramba kuzungukwa na mito mikubwa tunaomba ujenzi wa madaraja makubwa katika mito hiyo.” Aliomba Nchemba
Aidha Dkt Nchemba amemuomba Waziri mkuu apatapo chochote kilitwe kwa ajili ya ukarabati uwanja wa CCM iramba.
Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uwanja wa CCM Iramba Mkoa wa Singida. Picha na Hemedi Munga
Kaimu Mkuu Idara ya Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Lugano Sanga akijibu kero mbalimbali zinazohusu ardhi zilizowasilishwa kwa njia ya mabango mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uwanja wa CCM wilayani iramba Mkoa wa Singida.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.