Hemedi Munga, Irambadc
Iramba.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa Idara kutumia siku 4 kwenda vijijini kusikiliza kero za wananchi na kuwaelimisha kila mmoja katika sekta yake namna ambavyo watakavyoweza kunufaika kupitia idara yake.
Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo leo oktoba 6, 2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Tanzania wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na uwongozi wa awamu ya tano.
Akiongea na watumishi Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka watumishi kufahamu wajibu wao kwa wananchi kwa kuwa wananchi ndio wakuu wao. Huku akiwataka kufuata miongozo, taratibu na kanuni kwa kufuata falsafa ya mkuu wa nchi.
Serikali inataka watumishi wachapa kazi kwa kufuata miongozo, kanuni na taratibu, kuwa waadilifu na kuto kuwa na tabia ya wizi , udokozi, uwongo uwongo na kutoroka kazini. Mambo hayo hayana nafasi katika serikali hii. Aliongeza Waziri Mkuu.
Katika ziara hiyo amewakumbusha madiwani kuwa wanawajibu wa kusimamia shughuli zote na nini kifanyike katika halimashauri,usalama wa mali na fedha kuwa salama huka akiwataka kukemea mtu yoyote ambae hafuati utaratibu wa halmashauri hiyo kwa kuzingatia sheria za nchi na maelekezo ya serikali kuu. Aliongeza Waziri Mkuu
“Mmetafuta nywila (password) halafu mmeanza kubadilisha balisha takwimu katika mfumo wa mapato unaoitwa LGRCIS ambapo mmeishatafuna 150milioni huku akiwataja watumishi 10 ambao walikaa pamoja na kukubaliana kila hela inayioingia inakuwa ni yao” Alisema Waziri Mkuu
Kufuatia ubadhilifu huo Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa amewataka madiwani kuingiza katika baraza la madiwani kuwashughulikia watumishi 10 aliowataja.
Hata hivyo waziri Mkuu, kasim Majaliwa amemtaka kamanda wa Takukuru Mkoa kushughulika na watu 37 aliowataja waliohusika kujilipa posho 90 milioni toka katika pesa zilizoletwa kwa ajili ya kituo cha afya ndago na Kinampanda.
Waziri mkuu, Majaliwa amesifia jengo la macho lililojengwa hospitali ya wilaya ya Iramba kiomboi kwa shilingi 59 milioni na kutamani uzuri wa jengo hilo ndio ungekuwa uzuri wa kituo cha afya ndago.
Akiongea katika kikao hicho mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa afisa utumishi wa wilaya ya Iramba, B’hango Lyangwa amesema kuwa mwaka wa fedha 2018/2019 serikali imepandisha watumishi 793 madaraja na tayari baadhi yao wamekwisha ona mabadiliko ya stahiki zao.
Waziri Mkuu, Majaliwa aliwahakikishia watumishi kuwa serikali imeboresha ambapo mtumishi yeyote atakapopata barua ya kupanda daraja mabadiliko ya mshahara wake anaupata mwezi unaofuata.
Huku akiwataka watumishi kufahamu kuwa serikali inawapenda sana, inawajali hivyo waendelee kuwa watulivu na kuwa na Imani na serikali yao.
Waziri Mkuu, Majaliwa alimaliza mazungumzo yake na watumishi kwa kumsimamisha ukaimu Mweka Hazina wa wilaya ya Iramba bwana Hadhili Ngayunga mpaka pale takukuru watakapomaliza uchunguzi wao.
Kamati ya siasa, viongozi wa dini pamoja na watumishi wa umma wakufuatilia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa . Picha na Hemedi Munga.
Waheshimiwa madiwani na watumishi wa umma wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Picha na Hemedi Munga.
Watumishi wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.