Hemedi Munga, Irambadc
Iramba.Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harison Mwakyembe amekemea tabia ya baadhi ya waandishi wa habari kufanya usaili(interview) na viongozi mbalimbali baada ya hutuba zao.
Waziri huyo ameyasema hayo leo Ijamatano Januari 22, 2020 wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika kikao na Waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Madini mjini hapa.
Dkt, Mwakyembe amesema kuwa kufanya usaili baada ya hotuba ya kiongozi ni uzembe, uvivu na upotoshaji wa habari husika kwani kiongozi alikwisha zungumza katika hutuba yake hivyo si busara kufanyiwa usali tena.
Amesema kuwa kuna baadhi ya waandishi wa habari wakilalimika kuhusu kutokuwa na uhuru wa kupata habari ambapo alinukuu kipengele cha Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ibara ya 18 kifungu kidogo (d) ambacho kinasema
“kila mtu ana uhuru wa kupata taarifa wakati wowote”
Amesema wataalam wanaiona ibara hiyo kuwa ndio msingi wa kidemokrasia kutimiza haki ya wananchi kupata taarifa zilizokuwa sahihi.
“Ni wazi kuwa duniani kote tasnia ya habari haijaacha sekta binafsi kuwa na tafsiri ya uhuru wa habari usiokuwa na mipaka.
Aidha Waziri huyo ametolea mfano wa wakongwe wa habari kama Uingereza wa shirika lao la habari (BBC) kutangaza kwa lugha 40 ili kulinda dhima ya Taifa kimila na desturi.
“ Mwananchi anapaswa kupewa taarifa yenye kukidhi vigezo vyote vya taarifa sahihi,”alisisitiza na kuongeza Dkt, Mwakyembe
“Waandishi wa habari mnatakiwa kuyaeleza mazuri yanayofanywa na serikali ikiwa pamoja na Tanzania kuwa nchi ya kwanza kuingia kwenye teknolojia ya analogi na kwenda kwenye teknolojia ya digitali, hii imepelekea Tanzania kusifika katika taaluma ya mambo ya habari Barani Afrika ikifuatiwa na nchi ya Rwanda”
Pia kutimiza maslahi mapana ya wananchi kupata habari bila malipo na kulida tunu ya Taifa kwa kuzingatia maadili na desturi ya tasnia ya habari.
Aidha amewataka waandishi hao kufahamu sheria ya kupata habari (Access to information Act ) na ile ya Huduma ya vyombo vya habari (Media service Act ya 2016) ili kupata vigezo vya kua na weledi na maadili ya taaluma hiyo.
Amesema kufuatia sheria ya kupata habari, waandishi wa habari wametakiwa kufahamu kuwa kila taasisi inamsemaji wake mkuu hivyo inawapasa kuchukua taarifa sahihi na za uhakika kutoka kwa wasemaji hao huku wakilinda uhuru wa habari na kulinda maslahi, maadili ya nchi na usalama wake.
Kwa mujibu wa sheria ya huduma ya vyombo vya habari inawataka waandishi wa habari kuwa na weledi wa ngazi ya stashahada, digrii na kuendelea, ambaye atakosa sifa hizo, hatokuwa na sifa ya kuwa mwandishi wa habari.
Hata hivyo waandishi wa habari wametakiwa kuielewa nia ya serikali kuleta sheria hiyo ni kutaka kuwa na wanahabari wenye weledi na ujuzi mpana wa tasnia hiyo.
Vile vile Dkt. Mwakyembe ameahidi kufuatilia uwepo wa mtaala mmoja utakaotumika kwenye vyuo vyote vinavyotoa tasnia hiyo nchi nzima.
Akiwasilisha kero na changamoto za waandishi wa habari wa mkoa huo Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Singida Seif Takaza amemuhakikishia Waziri Dkt, Mwakyembe kuwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida wanafanya kazi kwa waledi mkubwa ingawa 99% ni waandishi wakujitegemea.
Waandishi hao wana changamoto yakutokuwa na mikataba ya kazi, kutolipwa vizuri na kwa wakati hali ambayo imesababisha kushindwa kujiendeleza kielimu kutekeleza matakwa ya sheria husika.
“Mhe, Waziri tunaishukuru serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na kuteuliwa kwako wewe kuwaWaziri wa tasnia hii ambayo imeshika kasi ya maendeleo, bila vyombo vya habari wananchi wasinge yaona maendeleo na sifa kemu kemu anazopata Rais wetu kupitia vyombo hivi, hivyo tunaomba serikali kupitia Wizara yako kuwasaidia wanahabari wanaotaka kujiendeleza kielimu ili kukidhi matakwa ya serikali ya kila mwandishi wa habari kuwa na kiwango cha elimu ya stashahada kwani waandishi wengi kipato chao hakikidhi kujisomesha wenyewe kwa kiwango wanachopata katika vyombo vyao wanavyovitumikia” amesema Takaza
Pia Mwenyekiti huyo ameiomba serikali kuzitambuwa klabu za waandishi wa habari kuwa taasisi muhimu kama zilivyo taasisi zingine, hivyo ameiomba serikali iwape maeneo ya kujenga ofisi za klabu ili kuepukana na kupanga nyumba za watu binafsi, kwani changamoto hii ni ya klabu za nchi nzima .
Halikadhalika Mwenyekiti huyo ameishukuru serikali kwa kuwaandalia mpango mzuri wa bima ya afya kwa waandishi wote ambao ni wanachama wa klabu za waandishi wa habari.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Habari Maelezo, Rodney Thadeus amewakumbusha waandishi wa habari umuhimu wa kuwa na kitambulisho (Press Card), kinachomtambulisha mwandishi wa habari na kuhifadhiwa kwenye kanzi data ya Habari Maelezo.
Pia ni rahisi kwa Mwandishi huyo anapokutwa na tatizo kusaidiwa kwa haraka na kutokusigana wakati anapotekeleza majukumu yake.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.