Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba ameahidi kuzipa kopyuta mpya za kisasa shule nne za Kata za Wilayani Iramba zilizofanya vizuri katika matokeo ya mwaka 2019 ikiwa ni motisha ya kuongeza ufaulu Wilayani humo.
Waziri huyo ametoa ahadi hiyo leo Jumanne 02, 2020 wakati akitoa salamu zake katika Baraza la Madiwani wa Halamshauri hiyo Ukumbi Mkubwa Mjini Kiomboi.
“Nitawapatia kompyuta mpya za kisasa hizo shule ili kuweza kusaidia taratibu hizi za kisasa za uandaaji wa masomo ya wanafunzi,” amesema Waziri Nchemba
Lengo likiwa ni kuwachochea Walimu kwa kazi nzuri wanazo zifanya chini ya usimamizi mzuri wa Mkuu wa Wilaya yetu, Emmanuel Luhahula.
Pia, amewaomba Madiwani kuwahamasisha watoto pindi shule zitakapofunguliwa kuwapa nafasi Walimu ambao wamefika Wilayani hapo kwa ajili ya kufundisha lugha mbalimbali za kitaifa na Kimataifa.
“Lugha ni ajira na wanaweza kupata soko kwa nchi ambazo zitakazohitaji mtu ambaye anajua lugha yao na Kiswahili kwakuwa Rais amekwisha kitangaza sana Kiswahili Kimataifa,” amesema Nchemba na kuongeza
“Yule atakaejua Kifaransa anaweza kupata ajira ukanda wakati, Kiarabu kwa ukanda wa kiarabu na Kireno kwa ukanda mwinge,”
“Pia, Taifa linahitaji wafanyabiashara wazalendo wakiwa wanaweza hizo lugha,watakua na uwezo wa kumudu biashara mbalimbali duniani.”
Akifafanua kuhusu ufaulu wa wanafunzi matokeo ya mwaka jana, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri hiyo, Godfrey Mwanjala amesema kuwa kompyuta hizo zitatolewa kwa shule ambazo zimekua zina vifaa hivyo vichache.
Mwanjala amezitaja shule hizo kuwa ni Kyengege Sekondari, Kisana Sekondari, Mgongo Sekondari na Kidaru ambazo zimeingia kumi bora kimkoa Singida.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya hiyo, Emmanuel Luhahula amewasifu Madiwani hao kwa kukubali na kulinda msitu wa Sekenge Tulya kuwa hifadhi.
Aidha ameonesha masikitiko yake kwa Watendaji kwa kuwa msitu huo unaendelea kuisha pamoja nakuwa ulipitishwa kuwa hifadhi.
“Watendaji wenzangu wa Serikali nendeni mkasimamie misitu hiyo kwa kuwa imekwishapitishwa kuwa ni hifadhi maana watu wanavuna misitu kama vile haina wenyewe,” amesikitika Luhahula
Halikadhalika, ameonesha imani yake kwa viongozi hao kuwa makini namna wanavyoshughulikia hoja na kuhakikisha Halmashauri hiyo inapata hati safi kwa miaka 5 mfululizo, hivyo kuacha historia ambayo haikuwako miaka michache iliyopita.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilayani humo, Ashery Joel amewaomba madiwani hao kuliangalia sana suala la usambazaji wa umeme warea vijijini.
“Ninaomba Mkurugenzi na Madiwani kuendelea kufuatilia usambazaji wa umeme warea kwa kua kuna baadhi ya maeneo baadhi ya kaya zimepata na baadhi hazijapata, hivyo hizo ni kero kwa mtu ambaye hajapata umeme kwati tumeambiwa kila mtu ataupata umeme,” amesema Joel
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula akifafanua jambo wakati alipokua akiongea na Madiwani pamoja na Watumishi mbalimbali Ukumbi Mkubwa wa Halmashuri hiyo mjini Kiomboi. Picha na Hemedi Munga
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Ashery Joel akiwaasa Madiwani kuhakikisha wanamaliza kipindi chao vizuri. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakifuatilia hoja mbalimbali Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri hiyo. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.