Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa akisalimia wananchi katika ziara ya kukagua mradi wa uchimbaji visima vya maji kata mgongo tarafa ya Shelui wilayani Iramba mkoani Singida.
Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo mafupi toka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Majitaka mkoani Singida (SUWASA) Mhandisi Patrick Mzamba juu ya mradi wa uchimbaji wa visima 3 vya maji katika kata ya Mgongo tarafa ya Shelui wilayani Iramba.
Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa amefanya ziara ya kukagua uchimbaji wa visima 3 vya maji kata ya Mgongo tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa ameongozana na Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Iramba Ndg. Dijovison Ntangeki, Kaimu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mhe: Samwely Shilla (Diwani wa CCM kata ya Ulemo), Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Ndg. Emmanuel Makwaya, waandisi wa maji ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida, waandisi wa maji wa wilaya ya Iramba na wataalamu mbalimbali katika ziara ya kukagua mradi wa uchimbaji wa visima kata ya Mgongo tarafa ya Shelui wilayani Iramba.
Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waheshimiwa madiwani wilayani Iramba na wanahabari mara baada ya kumalizia ziara yake ya kutembelea mradi wa uchimbaji wa visima 3 vya maji kata ya Mgongo tarafa ya Shelui, amemwaagiza mkandarasi pamoja na wataalamu wote wanaoshiriki kutekeleza mradi huo wasiwe kikwazo cha mradi huo kutokamilika kwa wakati na kufanikisha lengo la kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa Kiomboi.
“mradi huu ulitegemewa ukamilike kwa mwezi mmoja, sasa unachukua miezi mitatu, hii haikubariki kwa sababu kuna maeneo mengi watanzania wanahitaji kuchimbiwa maji na kwa mradi huu wananchi wamesubiri maji kwa mda mrefu, lazima mhakikishe kazi inamalizika kwa wakati na machine hii inahitajika kwenda kuchimba maji sehemu zingine alisema waziri Mbarawa.
Mradi huo wa uchimbaji wa visima 3 vya maji, tunategemea baada ya uchimbaji wa visima hivi kukamilika vitakuwa na uwezo wa kutoa takribani lita milioni 2.1 kwa siku. Nia ya serikali ni kuhakikisha watanzania wote wanapata maji safi na salama na ifika mwaka 2020 vijiji vyote tanzania vitapata maji safi na salama kwa asilimia 85 na maeneo ya mijini itapata maji kwa asilimia 100 alisema Profesa Mbarawa.
Aliongeza kusema “kuna mradi mwingine wa maji unatokea shinyanga kuleta maji Tabora, Igunga na tarafa ya Shelui ambao utagawa maji katika vijiji vyote vya Shelui ili kuhakikisha watanzania wanapata maji safi na salama.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.