Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhe. Selemani Jafo, amefanya ziara ya kushutukiza katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida na kutembelea ujenzi wa kituo cha Afya Ndago.
Akizungumuza na wananchi wa kata ya Ndago amesema,vimejengwa vituo vya Afya 208 kipindi cha Mwezi Januari 2018 hadi mwezi Mei 2018 Tanzania nzima vyenye Thamani ya shiling bilioni156 na vimeongezwa vituo vya Afya 97 na kila kituo cha Afya nchini pamejengwa jengo la mama na watoto, Majengo ya upasuaji, Maabara, Nyumba ya Daktari, Mortuary na walkways.
Vile vile amemshukuru Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba kwa kuchangia mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Ndago.
Aidha katika ziara hiyo waziri Jafo ametembelea na kukagua ujenzi wa barabara yenye kilometa saba (7km) kutoka Kyengege hadi Makunda Kata ya kyengege wilaya ya Iramba mkoa wa Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula akimpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa (Tamisemi), Mhe. Selemani Jafo kwenye ziara kukagua ujenzi wa kituo cha Afya Ndago.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.