Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewasha rasmi umeme katika kijiji cha New Kiomboi kata ya Kiomboi wilayani Iramba mkoa wa Singida leo Tarehe 15 Desemba 2018.
Mhe. Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara hiyo ya kukagua utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini (REA) Wilayani Iramba mkoa wa singida akiambatana na Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl Linno Mwageni, Viongozi mbalimbali kutoka REA, TANESCO, Wakandarasi pamoja na wananchi.
Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha New Kiomboi, Waziri Kalemani amesema “Leo nimekuja kuwasha umeme na kukagua utekelezaji wa mradi wa REA mkoani Singida.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Kalemani alisema kuwa mkoa wa Singida umepewa wakandarasi 3 kwa lengo la kuhudumia wananchi kwa haraka kupeleka umeme kwenye vijiji 247 vya mkoa wa singida pamoja na vitongoji vyake Kuwa ndani ya miezi 12 ijayo vijiji vyote viwe vimewashwa umeme na vitakuwa vimebaki vijiji 87 ambavyo vitafungiwa umeme kuanzia Julai mwakani. “Wakandarasi hawa watafunga umeme Kijiji kwa Kijiji, Kitongoji kwa Kitongoji, Nyumba kwa Nyumba bila kuruka nyumba yoyote” alisisitiza Waziri Kalemani.
Amewaasa wananchi kulipia Shilingi 27,000/= ili wafungiwe umeme manyumbani mwao na hakuna nyumba kurukwa hata kama ni nyumba ya makuti au nyasi aliongeza kusema.
Waziri Kalemani amehimiza Ofisi ya Mkurugenzi, kuhakikisha Taasisi zote za Umma., Vituo vya afya, Makanisa, Misikiti, Zahanati, kutenga fedha kwa ajili ya kuunganishia umeme “Yale maeneo ya Taasisi, vituo vya afya, misikiti, makanisani, shule zote, zahanati zifungiwe umeme kwa gharama ya shilingi 27,000/=” alisema waziri Kalemani.
Aidha amewaasa wananchi kutumia vifaa vya umeme Tayari (UMETA) 250 vilivyotolewa bure na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa wananchi watakao wahi kuunganisha umeme manyumbani kwao.
Vile vile waziri Kalemani amewachangia wananchi wa Kijiji cha New Kiomboi vifaa vya umeme Tiyari (UMETA) 20 ili kuunga jitihada zao za kuingiza umeme manyumbani mwao “Kwa kuwa gharama za kufunga wiring ni kubwa wananchi wekeni vifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ambavyo havihitaji wiring na vinaweza kuwasha vyumba vitatu, Firiji, jiko la umeme, pass na simu. Ninapenda kuwaamasisha wananchi kutumia hivyo vyombo vinaharakisha kupata umeme na atakayechelewa kufunga umeme na vikaisha utalazimika kununua kwa Shilingi 36,000/= alisema waziri Kalemani
Amemtaka meneja wa kanda ya kati kuhakikisha anasimamia vifaa vya kusambaza umeme Wilayani Iramba. “Kama wewe umesoma hapa akikisha wananchi wa Iramba wanapata umeme, wewe unauwezo wa kutafuta nguzo, transfoma na vifaa vingine sehemu yeyote. Hakikisha vijiji vyote na vitongoji wilayani Iramba vinapata umeme alisisitiza waziri Kalemani.
Amemwagiza meneja wa Tanesco wilaya ya Iramba kuwatembelea wananchi ili kujua mahitaji yao ya umeme. “Kuanzia leo anza kutembelea wananchi ili kujua mahitaji yao ya umeme na hakikisha unaanzisha vituo vidogo vidogo ambapo kuna wananchi wengi ili waweze kupata huduma kwa urahisi. Kila kijiji weka genge la wafanyakazi na tumia vibarua kuharakisha kazi. Hakikisha mnaweka vituo ili wananchi waweze kulipa. Ni marufuku mkandarasi kutoa vibarua nje ya mahali wanapofanyia kazi”. alisema waziri Kalemani.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula alimshukuru sana Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kusema kuwa wananchi wa Iramba wanahitaji umeme ili kuendelea kufungua Viwanda vidogo vidogo na hata kuboresha kipato cha kiuchumi katika miongoni mwao.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika Kijiji cha New Kiomboi Kata ya Kiomboi wilaya ya Iramba leo Tarehe 15 Disemba 2018.
Wananchi wa kijiji cha New Kiomboi kata ya Kiomboi wilayani Iramba wakisalimiana na waziri Kalemani.
Mkuu wa Wilaya wa ya Iramba mkoani Singida Mhe. Emmanuel Luhahula akizungunza na wakazi wa Kijiji cha New Kiomboi katika mkutano wa uwashaji umeme mradi wa umeme wa REA vijijini.
Baadhi ya wanakijiji cha New Kiomboi wilayani Iramba wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani.
Waziri Mhe. Dkt Merdard Kalemani akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi wa shule ya sekondari New Kiomboi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.