Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe:Emmanuel Luhahula akiambatana na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni leo wamezindua zoezi la utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV) ambayo inatolewa kwa Wasichana waliotimiza umri wa Miaka 14. Mkuu wa Wilaya ya Iramba amesema zoezi hilo limeanza leo April 27, 2018.
Vile vile wamezidua mpango wa chanjo ya polio kwa njia ya sindano (IPV) utoaji wa chanjo ya sindano ya kuzuia ugonjwa wa polio kwa watoto wenye umri wa wiki 14.
Chanjo hii inaanza kutolewa kwa njia ya matone mtoto anapozaliwa, anapofikisha wiki 6, wiki 10 nawiki 14.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Iramba amesema utoaji wa chanjo hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na ugonjwa wa saratani ambao umekuwa ukisababisha vifo vya kinamama wengi huku akiitaka jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara.
Pamoja na hayo Mkuu wa Wilaya ya Iramba ametoa wito kwa viongozi wa dini, madiwani, wenyeviti wa Vijiji na wajumbe wa kikao kuhamasisha jamii kuwapeleka watoto wao zahanati au hospitali kupata chanjo hiyo. Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Iramba amesema chanzo cha ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na mapenzi katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, kuzaa watoto wengi pamoja na uvutajiwa sigara ambapo dalili zake ni kutokwa na damu bila mpangilio, maumivu ya mgongo, miguu, kiuno, kutokwa na uchafu ukeni pamoja na kuchoka, kupungua uzito na hamu ya kula.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Dkt.Boniface Marwa ametoa Ufafanuzi akisema Saratani ya mlango wa kizazi inasababishwa na virusi vya Human Papilloma ambapo tiba yake kwa hatua ya mwanzo ni kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini dalili za mwanzo na kupata matibabu stahiki.
Vilevle amesema Saratani ya mlango wa kizazi ni saratani ambayo hutokea kwenye via vya uzazi wa mwanamke ambayo ni kiingilio kutoka uke hadi katika mfuko wa uzazi. nimoja kati ya zaidi ya aina 40 ya virusi vya human papilloma (HPV), ambavyo 13 vinasababisha saratani.
Matibabu kwa wagonjwa walio na virusi hivyo yanategemea na viwango vya virusi hivyo mwilini, hata hivyo yanaweza hitaji kutibiwa kwa njia ya upasuaji na kutoa sehemu au mfuko wa uzazi mzima au kutumia miyonzi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.