ZAIDI YA BIL. 1.59 ZA MRADI WA BOOST KUONDOA CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU YA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA KATIKA SHULE ZA MSINGI WILAYANI IRAMBA”
Jumla ya vyumba vya madarasa 18 na matudu ya vyoo 18 vinatarajiwa kujengwa katika maeneo mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ili kupunguza upungufu na msongamano wa wanafunzi kupitia mradi mpya wa Boost utakaogarimu Kiasi cha shilingi 1,590,000,000/=
Akizungumza wakati akifungua kikao cha Kutambulisha mradi huu kwa wajumbe kutoka shule ambazo zimepata bahati ya kutekeleza mradi huu wa Boost Leo tarehe 04 aprili 2023 Afisa Tarafa ya Kisiriri Bw. Oswald Leopold kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleimani Yusuph Mwenda amesema,
“Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita chini ya Raisi wetu Dkt Samia Suluhu Hasani kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kutuletea mradi huu wa Boost ambao unakwenda kumaliza changamoto ya miundombinu katika sekta ya Elimu kwa kukarabati na kujenga miundombinu ya shule kwa elimu yaa awali na msingi”.
*Niwaombe sana wajumbe kila mmoja kwa nafasi yake akatimize majukumu yake na kuhakikisha mradi huu wa Boost unakamilika kwa wakati na unakuwa na ubora unaostahili, Na mradi huu sasa tutakwendas kulipwa kulingana na matokeo yani kama tutamaliza kwa wakati na madarasa yakawa na viwango vinavyohitajika tutakua na firsa ya kuongezewa fedha zingine kwaajili ya kukarabati na kujenga miundombinu mingine kwa shule ambazo bado zina uhitasji lakini kama hatutamaliza kwa waskati maana yake tutaziba fursa ya kuendelea kupata fedha za mradi huu wa Boost. Alisisitiza Bw. Oswald
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.