Na Hemedi Munga
tehama@irambadc.go.tz
Singida - Iramba. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewaagiza Wahandisi wote kuwasimamia kikamilifu mafundi ujenzi ili waongeze nguvu za vibarua hatimaye wakamilishe ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa wakati.
Dkt. Mahenge ametoa agizo hilo leo Jumatatu Aprili 12, 2022 wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la Dharura na ICU katika Hospitali ya Kiomboi wilayani Iramba mkoa wa Singida.
“Tunataka jengo lote lionekane kuna watu wanafanya kazi, hivyo msimamizi anayesimamia ujenzi huu aongeze nguvu nakutoa fedha kwa vibarua hao.” Alisema Mkuu huyo wa Mkoa
Aidha, aliongeza kuwa ni lazima tusimamie fedha hizi vizuri ili matunda yaliokusudiwa yafikiwe kwa sababu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezitafuta fedha hizi ziwanufaishe watanzania.
Katika hatua nyingine, Dkt. Mahenge alimshukuru Rais Samia kwa kuleta fedha zaidi ya Tshs 232 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Singida ikiwemo ujenzi wa shule mpya, madarasa mapya, zahanati, vituo vya afya,ICU, maji na barabara.
Pia, alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda kwa namna alivyoshirikiana na watumishi wote wa wilaya hiyo kusimamia miradi ya maendeleo.
“Ninawapongeza watumishi wote wa wilaya ya Iramba kwa sababu miradi hii inakwenda vizuri.” alipongeza na kuoneza kuwa
“Ni wajibu wetu kusimamia na kufanya ukaguzi wa miradi hii kwa sababu ni fedha nyingi zimeleekezwa katika miradi hii mikubwa, hivyo ni lazima tuisaidie serikali.”
Kufuatia uwepo wa fedha za kushughulikia miradi ya maendeleo, alimtaka Mhandisi Profil Modaha kutimiza wajibu wake na kupata uzowefu kutoka katika Idara ya maji kwa namna wanavyosimamia miradi yao vizuri.
“Mhandisi! hili nililoliona sijalipenda na nitaanza kukuchunguza ili kubaini kuwa kiti hicho ulichokalia kiko sawasawa.”
Akiongea katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Iramba, Suleimana Mwenda alimpongeza meneja wa RUWASA Iramba, Mhandisi Ezra Mwacha kwa namna anavyosimamia miradi ya maji na kubakiza bakaa katika kila mradi anaousimamia.
Aidha, Mwenda alimshukuru Rais Samia kwa kuwajali wananiramba kwa sababu wamepata miradi ya maendelo mingi.
Alisema kuwa ukiachilia mbali miradi ya afya, ICU, jengo la dharura, Vituo vya Afya, zahanati, ujenzi wa shule mpya, madarasa na barabara Iramba imepata mradi wa maji toka ziwa Viktoria Kupitia Shinyanga Tinde wenye gharama ya Tshs 24 bilioni.
Wakiongea na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti wananchi wa Iramba na mafundi wamempongeza na kumuombea afya njema Rais Samia ili aendelee kuliongoza Taifa hili na kuendelea kuwakumbuka kuwaletea miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Kapula Kashindi mkazi wa Mwanza alimshukuru Rais Samia kwa miradi hii ya maendeleo kwa sababu imemuwezesha yeye kupata ajira na hivyo kujikuta akiwa Iramba.
“Kwa kweli tunamshukuru sana Rais Samia maana miradi hii ndio imenifanya niwepo hapa kwa sabubu bila miradi hii nisingekuwa hapa.” Alithibitisha
Naye Adamu Kitundu alisema kuwa mwanzoni huduma ya Afya ilikuwa unaipata umbali mrefu hasa kwa akinamama wajawazito pindi wanapokuwa wameshikwa na uchungu lakini kwa sasa kila hatua chache utakuta kutuna kituo cha Afya na hivyo kuokoa uhai wa wananchi.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge ilifika na kukagua ujenzi katika kituo cha Afya Kisiriri kata ya Kisiriri, ujenzi wa jengo la dharura na ICU kata ya Oldi Kiomboi, ujenzi wa Shule mpya na mradi wa maji kata ya Maluga wilayani Iramba.
MWISHO
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.