Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida , limepitisha Kwa kauli Moja rasimu ya bajeti ya mapato na matumizi Jumla ya shilingi bilioni 34.9 Kwa Mwaka Mpya wa fedha ujao 2024 -2025 katika kikao Maalumu Cha Baraza la Madiwani kilichoketi Machi 07 Mwaka huu katika Ukumbi mkubwa wa mikutano katika Halmashauri hiyo.
Akisoma Bajeti hiyo Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Gunnah Charles Maziku Amesema kuwa Halmashauri ya Iramba imeweka makisio hayo kutoka na kupata fedha hizo katika vyanzo mbali mbali ikiwemo Mapato ya ndani kiasi Cha Tsh. BL 3.6 mishahara bilioni 18.7Matumizi mengineyo bln1.1miradi ya maendeleo Ruzuku kutoka Serikali kuu , bilioni 5. 6 na miradi ya maendeleo Kwa fedha za wahisani bil 5.7 na kufanya jumla ya makisio kuwa ni Bilioni 34.9.
Aidha Kwa Upande wa matumizi pia Maziku Amesema kuwa Halmashauri imekisia kutumia jumla ya shilingi bilioni 34.9 kutokana na vyanzo mbali mbali vya Mapato; Amesema Upande wa Mapato ya ndani Kwa Upande wa mishahara Halmashauri itatumia Tsh million 23.3 matumizi ya Kawaida Tsh milioni 2.1 miradi ya maendeleo Kwa Mapato huru ni milioni 448.6 miradi ya maendeleo Kwa Mapato fungwa ni Bilioni 1,044,000,391.54 Kwa hiyo na kufanya kuwa na Tsh bilion 3.6 ambayo itatumika Kwa Mapato ya ndani.
Maziku Amesema kwa Upande wa Ruzuku ya Serikali Kuu Halmashauri imekisia kutumia jumla ya shilingi bilioni 18.7kwa ajili ya mishahara matumizi ya kawaida bilioni 1.1 miradi ya maendeleo bilioni 5.6 na wahisani mbalibali bilioni 5.7 na kufanya jumla yamatumizi ya Bilioni 34.9.
Akitoa salamu za Serikali Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda Amesema kuwa Ili shughuli za Serikali ziweze kwenda kwa Ufanisi mkubwa Bajeti ni kitu muhimu sana, " Bajeti ndiyo itakayo tuambia tunaend kutekeleza miradi mingapi katika sekta mbali mbali iwe Elimu , Barabara, maji, liwe Umeme Afya na nyinginezo". Amesema DC Mwenda.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.