Mgeni rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda,ametoa zawadi mbalimbali ,ikiwemo fedha taslimu kwa wanafunzi 10 waliofaulu vizuri katika mtihani wa Kumaliza elimu ya Msingi (Darasa la Saba), Walimu waliofaulisha vizuri katika masomo yao, Shule zilizoongeza ufaulu, Shule zilizoongoza kwa Kata kupewa motisha za Kompyuta ;
Zawadi nyingine ni kwa Shule Bora 6 zilizoongoza Kiwilaya pia Kata zilizoongoza Kiwilaya kwa ufaulu, Kata zilizoongeza ufaulu kwa kiasi kikubwa Kiwilaya, Shule binafsi zilizoongoza ufaulu Kiwilaya na shule iliyoongeza ufaulu kwa kiasi kikubwa sana Kiwilaya (Mwamapuli iliyopo Kata ya Kidaru)
"Kuongeza ufaulu kwa darasa la Nne na darasa la Saba katika Shule, katika Kata, Ni kazi kubwa na juhudi kubwa Sana Hongereni sanasana ,Tangu niwe Mkuu wa Wilaya hapa, nilikuta kiwango cha ufaulu kilikuwa alama 58 lakini mmejitahidi ndani ya Miaka 3 kuongeza asilimia za ufaulu kutoka 58 na sasa ni 71.9" Amesema Mwenda.
"Lengo letu ilikuwa ni kufikia asilimia 85 lakini kwa sasa Mkuu wa Mkoa amekuja na lengo lake, na Kwa kuwa Mkuu wa Mkoa ni kiongozi wetu wa Mkoa yeye amelenga kufikia asilimia 90 hivyo Naamini kwa msimu huu tutajitahidi tufikie lengo hili " Amesisitiza Kiongozi huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Michael Matomora amesema, yeye na menejimenti yake wameona ni vema kuwamotisha Walimu kutokana na kazi kubwa ya kutoka kwenye nafasi ya Mwisho katika Mkoa. Pia Kuongeza alama ingawa bado tunatakiwa kushika nafasi tatu za juu zaidi.
Mwenyekiti wa huduma za Jamii Wilfred Kizanga, Amewataka Walimu kishirikiana na kuondoka katika nafasi za Mwisho kwani Iramba siyo Mrithi wa nafasi hizo, Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi, Amewataka Maafisa Elimu Kata kuvua vyeo vyao na kishirikiana na Walimu, Vilevile Walimu wakuu nao vivyo hivyo kwa ushirikiano huo, Iramba itashika nafasi tatu za kwanza Kimkoa
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.