Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mheshimiwa Innocent Msengi Agosti 13,2024, imefanya ziara ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo ya miundombinu ya elimu na afya katika wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo Wajumbe hao waliambatana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Lengo la ziara hiyo likiwa ni kutathmini maendeleo ya miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaokubalika.
Wakati wa ziara hiyo, kamati ilikagua miradi mbalimbali ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Kaselya na Shule ya Msingi Urughu, Ujenzi wa Matundu 5 ya Vyoo,Kichomea taka na mnara wa maji katika zahanati ya Kaselya.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mhe. Innocent Msengi amewapongeza Wataalamu wa Halmashauri na wasimamizi wa Miradi kuhakikisha Miradi inatekelezwa kwa ubora ili iweje kudumu muda mrefu na kutoka huduma Bora kwa wananchi.
"Tumefurahishwa na maendeleo ya miradi hii," alisema Mhe. Innocent Msengi. "Tunawaagiza wasimamizi wa miradi hii wahakikishe inakamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu. Tunataka wananchi wa Tunduru waanze kunufaika na miradi hii haraka iwezekanavyo."Alisema Mheshimiwa Msengi.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango pia walipongeza mwenendo wa ujenzi wa miradi hiyo na kuwataka wasimamizi wahakikishe kuwa inajengwa kwa uadilifu na kwa uwazi. Walisisitiza pia umuhimu wa ushirikiano kati ya kamati za ujenzi na wananchi katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa mafanikio.
Aidha ziara hii ni sehemu ya juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ya kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kwa uwazi. Halmashauri inaamini kuwa miradi hii itaboresha maisha ya wananchi wa Iramba kwa kiasi kikubwa.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.