Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amefanya ziara ya kutembelea na Kukagua mradi wa Ujenzi wa vyumba Vitatu vya madarasa na matundu 10 ya Vyoo Shule ya Msingi Kipuma.
Serikali kupitia Mradi wa BOOST imetoa jumla ya shilingi Milioni 79,000,000 kwa ajili wa Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa kwa gharama ya Shilingi Milioni 69,000,000 na Ujenzi wa matundu Sita ya Vyoo kwa gharama ya shilingi Milioni 10,000,000
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Iramba aliambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama,Wakuu wa Taasisi za Umma zilizopo Wilayani Iramba,Wakuu wa idara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Ngud. Michael Agustino Matomora.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.