Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula, amefanya ziara leo tarehe 20.03.2019 katika kijiji cha Nsonga, kata ya Kaselya Tarafa ya Ndago.
Akiwa katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo, amefika katika Kijiji cha Kaselya, Kata ya Kaselya kutazama shamba la Bwana Salehe Juma aliyepanda miche ya mikorosho 130 hekari nne na nusu iliyotolewa bure na Mhe Rais, John Joseph Magufuli.
Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula, amempongeza sana na kusema kua Bwana Salehe Juma ni mfano wa kuigwa na kuwataka watendaji wa vijiji kuwasaidia wakulima ili wachungaji wasichungie mifugo katika mimea hiyo.
Naye Salehe Juma amewataka wakulima kuto kukata tamaa, wasiogope, wasubutu kupanda mikorosho kwani mikorosho itakua na watapata soko la korosho.
Mhe, Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Luhahula akikagua shamba la Mhe. Diwani wa Kata ya Kaselya, Charles Dagau aliyepanda Alizeti ya Hyssum 33 iliyohamasishwa na Mhe, Mkuu wa Mkoa, Daktari Rehema Nchimbi.
“Nitoe wito kwa viongozi wengine, Waheshimiwa Madiwani na Watumishi wa Umma wote kuiga mfano wa kilimo hichi kwa kuwa Mhe, Mkuu wa Mkoa, Daktari Rehema Nchimbi anahamasisha tulime Alizeti aina ya hyssum 33 na hii ni alama ya Iramba,” amesema
Akizungumza Mhe, Diwani wa Kata ya Kaselya Tarafa ya Ndago, amehamasika kulima Alizeti hiyo kutokana na uhamasishaji unaofanywa na Mhe, Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Luhahula, kuwataka wananchi walime kwa wingi kilimo cha Alizeti.
“Ninatumia mbolea ya samadi ambayo inauwezo wa kukaa miaka mitatu na ninapokua na mikutano wakati wowote ule ninawahamasisha wananchi wabadilike angalau waachane na mazao yale yanayowapa hasara, natayari wananchi wengi katika kata yangu wanatumia mbegu hii mpya,” amesema
Mhe, Diwani wa Kata ya Kaselya Tarafa ya Ndago amesema, Nimelima hekari 10 za hyssum 33, mahindi hekari 10 na miche ya korosho hekari 10, ninatoa wito kwa jamii katika mazingira yanayokwenda na tekenolojia ya kisasa, tunahitaji kufuata wataalam wanavyotuhamasiha kuwaunga mkono tulime zao la korosho ili litusaidie katika maisha ya baadae.
Akihitimisha ziara yake katika Kata ya Kaselya, Tarafa ya Ndago Mhe, Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Luhahula amewataka viongozi kusimamia miradi ya maendeleo kwa uadilifu na kuhakikisha wafugaji wanawaheshimu wakulima kwa kutoingiza mifugo kuchungia katika mashamba ya Alizeti, Mahindi na Miche ya Mikorosho.
Habari na Hemedi Munga
Mhe, Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Luhahula (wakwanza kulia) akikagua shamba la Mhe, Diwani wa Kata ya Kaselya, Charles Dagau aliyepanda Alizeti ya Hyssum 33 iliyohamasichawa na Mhe, Mkuu wa Mkoa, Daktari Rehema Nchimbi. Picha na Hemedi Munga.
Mhe, Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Luhahula (wapili kulia) amefika katika Kijiji cha Kaselya, Kata ya Kaselya kutazama shamba la Bwana Salehe Juma aliyepanda miche ya mikorosho 130 hekari nne na nusu iliyotolewa bure na Mhe Rais, John Joseph Magufuli. Picha na Hemedi Munga.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.