Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amefanya ziara na kufanya mkutano wa hadhara kuongea na wananchi, kusikiliza kero na kuhamasisha shughuli za maendeleo kijiji cha Kikonge, kata ya Mbelekese Tarafa ya Ndago leo tarehe 22.03.2019.
Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amewataka wananchi kudumisha usafi wa mazingira na kuwataka wazazi kuacha tabia ya kuwalea wanafunzi watoro.
“Niliagiza kila kaya na taasisi zote kujenga choo bora na watendaji wote kukomesha suala la utoro shuleni, endapo atakapopatikana mwanafunzi mtoro kamata mzazi wake ili tuzalishe watoto wasomi na hatutaki kuzalisha wajinga,” amesema
Akiongea Mhe, Mkuu wa Wilaya katika kikao kazi na wataalam mbalimbali amewataka washirikiane vizuri ndipo wataweza kuleta maendeleo kata ya mbelekese.
“Kwenye kata hii hakuna ushirikiano wa watumishi wa umma, ushirikiano ni mdogo, hatuwezi tukaendesha kata kwa kutokua na ushirikiano tudumishe ushirikiano ili tulete maendeleo kata ya Mbelekese,” amesema.
Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amewapa miezi miwili Maafisa Tarafa, na Kaimu Kamanda wa takukuru wilaya, Benjamin Masiyaga kuhakikisha wilaya yote viongozi wanasoma mapato na matumizi na atakaye shindwa kutekeleza atakua hatoshi.
Akiongea katika kikao kazi Shekhe wa Wilaya ya Iramba, Athumani Hussein amemuomba Mhe, Mkuu wa Wilaya kuwahimiza viongozi kusoma mapato na matumizi kwa wananchi ya fedha mbalimbali wanazozikusanya ili kuwajengea Imani ya kufaham fedha iliyochangwa na namna ilivyotumika.
Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula, akiongea na viongozi wa mazehebu mbalimbali ya dini ya kikristu na kiislam kuwashukuru kwa heshima wanayompa Mhe, Mkuu wa Wilaya kwa kuiombea Wilaya ya Iramba iwe salama.
Akiongea na viongozi wa mazehebu katika suala la ulinzi na usalama amewaomba viongozi wa dini kuisadia serikali kuwafichua wale wote wanaotumia makanisa au misikiti kufanya maovu.
“Niwaombe viongozi wa dini mtusaidie kuwa makini kuwafichua watu wanaotumia vyombo vya dini kufanya maovu. Nilazima viongozi wa dini tulinde amani yetu na kudumisha kulinda amani ya wilaya yetu,” amesema
Naye Mhe Diwani wa kata ya Mbelekese amemkabidhi Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula madawati 146 shule ya sekondari Mbelekese, yanayotokana na juhudi zake za kuhamasisha maendeleo na kukuza ufaulu wa wanafunzi.
Akiongea mbele ya Mkuu wa Wilaya Elizabeth Emmanuel, mwanafunzi wa shule ya Sekondari Mbelekese kidato cha kwanza amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwakabidhi wanafunzi madawati hayo yanayotatua changamoto walizokua wanazipata na kuwaomba viongozi waendelee na moyo huo huo wa upendo.
Akitoa shukran Mchungaji, Joseph Masensi wa Usharika wa Ndago, amesema wanafurahi sana kwa ushirikiano wanaopatiwa na Mhe, Mkuu wa Wilaya, aidha amemuomba kulitazama upya suala la upatikanaji wa mkaa kwa kua imekua ni changamto kubwa wanaipata kwa sasa.
Habari na Hemedi Munga
Naye Afisa Ardhi, Kennedy Thobias Mpanduji kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, amewakabidhi mwalimu na uongozi wa shule madawati 146 na kuwaomba kuwa na usimamizi mzuri. Aidha amewataka wanafunzi wayatumie vizuri ili baada ya miaka ijayo wadogo zao watakapo kuja wasipate tabu ya madawati na uongozi usichangie tena madawati ispokua wachangie vitu vingine vya maendeleo ya shule ya sekondari Mbelekese. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.