ZIARA YA WAH MADIWANI WAJUMBE WA KAMATI YA FEDHA, MIPANGO NA UTAWALA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO TAREHE 23 JANUARI, 2023
Kamati ya Fedha Mipango na Utawala imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Kamati inafanya hivyo kwa mujibu wa kanuni ya 44(3) ya kanuni za kudumu ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, 2013 zikisomwa kwa pamoja na jedwali la kanuni sehemu A kipengele cha (i) cha kanuni za kudumu za Halmashauri ya Wilaya , 2013.
Kamati ya Fedha Mipango na Utawala imetembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa Shule ya Sekondari ya Kidaru unaojengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu, mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Tyegelo kwa kutumia fedha za Tozo, ukamilishaji wa vyumba vya madarasa mawili na ofisi tatu katika sekondari ya Ntwike unaojengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu ,ujenzi wa zahanati ya wembere kupitia Globa Fund. katika Kata ya Shelui na ujenzi wa Sekondari ya Dkt. Mwigulu
MRADI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA VINNE (4) KATIKA SHULE YA SEKONDARI KIDARU
Kamati ilitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili na ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Kidaru. Wajumbe wa kamati walipongeza uongozi kwa usimamizi mzuri wa miradi kwani inaridhisha.
MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA TYEGELO
Kamati imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Tyegelo ambapo kuna ujenzi wa mradi wa jengo la OPD, Jengo la maabara, jengo la kichomea taka, jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji na jengo la kufulia kupitia fedha za Tozo. Wajumbe wa kamati walipongeza uongozi wa Kijiji ,uongozi wa Kata na Kamati ya Ujenzi kwa usimamizi mzuri wa miradi. Vile vile Wajumbe wa Kamati wameagiza ifikapo Februari, 2023 majengo yawe yamekamilika na Kituo kianze kufanya kazi.
MRADI WA UKAMILISHAJI WA UJENZI WA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA YENYE OFISI KATIKATI SHULE YA SEKONDARI NTWIKE.
Mradi wa ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa yenye ofisi katikati na Ofisi ya walimu ulianza kutekelezwa kuanzia tarehe 04 Oktoba, 2022 ambapo madarasa mawili na Ofisi katikati imekamilika,
MRADI WA UJENZI WA ZAHANATI WEMBERE
Mradi wa ujenzi wa zahanati mpya katika Kijiji cha Wembere, Serikali imetoa fedha kupitia Globa Fund ili kuwezesha kujenga Zahanati hii baada ya wananchi wa Wembere na Tintigulu kupata changamoto ya huduma ya afya kwa muda mrefu. Wajumbe walisisitiza mafundi wahimizwe waweze kukamilisha mradi haraka kwakuwa vifaa vipo ili huduma ianze kutolewa kwa wananchi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.