Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amewataka Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kata ya Mtoa Wilayani Iramba wametakiwa kuzingatia uzalendo,Uadil na kuwa chachu ya Maendeleo katika jamii wanayoishi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Yusuph Mwenda wakati akifunga rasmi mafunzo hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Tyeme Novemba 15,2024
Mwenda amewapongeza wahitimu wote na kuwasihi kuyatumia mafunzo hayo kama chachu ya kujiletea maendeleo na kuhakikisha kuwa wanailinda jamii inayowazunguka. Aidha, amewaahidi kuwa Serikali ipo nao bega kwa bega na ndiyo maana imetumia gharama kubwa kuwapatia mafunzo hayo.Hata hivyo Mwenda alitumia fursa hiyo kuyaagiza makampuni binafsi ya ulinzi kuwatumia vijana hao wenye mafunzo ya kijeshi kwa shughuli zao za ulinzi.
Aidha Mwenda ametumia fursa hiyo kuwaasa vijana wilayani humo kuwa inapotokea fursa kama hiyo katika Kijiji chochote wajitokeze kwa wingi na wasikatishwe tamaa kwani Serikali inatumia gharama kubwa kufanikisha mafunzo hayo.
"Vijana wangu najua mmepitia vikwazo vingi na ninajua mlikatishwa tamaa maana wapo mabingwa wa kukatisha watu tamaa lakini mmevuka salama na leo mnahitimu, basi mafunzo haya yawe na tija katika maisha yenu binafsi na jamii inayowazunguka". Anasema Mwenda.
Mafunzo hayo ya miezi 3 Awali yalijumuisha vijana 126 yalianza Julai 1,2024 na kufunguliwa Agosti 14,Hata hivyo wanafunzi 39 hawakuweza kuendelea na mafunzo kutokana na kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kujitolea,Wanafunzi 10 waliacha mafunzo wenyewe kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kubezwa na kukatishwa tamaa na Jamii, ambapo Waliohitimu ni 80 kati ya hao wanaume 67 na wanawake 13 chini ya usimamizi wa Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Iramba Meja Eusebi Mtesigwa.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.