Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleimani Yusuph Mwenda ameongoza Wakuu wa divisheni na vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba,Wananchi wilayani hapa kupanda miti 3500 katika Vijiji vya Kizonzo na Mseko vilivyopo Kata ya Mgongo ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya upandaji miti kwa Wilaya ya Iramba yenye lengo la kuifanya Iramba iwe ya kijani.
Akizungumzia siku hiyo Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleimani Yusuph Mwenda ,amesema siku ya Upandaji miti imelenga kuiweka Pamoja Viongozi na Wananchi ili kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii, ambapo aliwataka Wananchi kutoa ushirikiano katika kubaini vitendo vya kihalifu katika jamii.
Aidha, DC Mwenda. amewataka Wananchi wa Vijiji hivyo kutunza Miti iliyopandwa leo Machi 9, 2023 ili ilete tija kwao na kwa kizazi kijacho
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mkuu wa divisheni ya rasilimali watu amesema kuwa maelekezo ya Kitaifa ni kuhakikisha kila Wilaya inapanda Miti isiyopungua Milioni moja na Laki tano(1,500,000) na kila Kaya kupanda Miti isiyopungua Minne(4) ambapo aliwataka Wananchi kutumia jitihada binafsi katika kufanikisha zoezi hilo.
Afisa Mtendaji Kata ya Mgongo ,Maria Daudi ametaja umuhimu wa zoezi hilo na kueleza mikakati watakayochukua kutunza Miti hiyo ikiwemo kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atakaye bainika kubeza juhudi za Serikali zinazolenga kupambana na mabadiliko ya Tabia Nchi.
Hii ni awamu ya Tatu ya zoezi la upandaji Miti Wilayani hapa ambapo zoezi la kwanza lilianza siku ya uhuru wa Tanganyika, awamu ya pili ilizinduliwa hivi karibu na Mkuu wa Mkoa wa Singida na leo ni awamu ya Tatu ambapo jumla ya miti Elfu tatu na mia tano(3500) Kata ya Mgongo vijiji vya Mseko na Kizonzo
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.