Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ameweka jiwe la ufunguzi kwenye jengo la kutolea huduma za macho hospitali ya wilaya Kiomboi wilayani Iramba leo tarehe 10.10.2019 Katika kuadhimisha siku ya Macho Duniani,
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula akiongea na wananchi siku ya kuadhimisha siku ya macho duniani katika hospitali ya wilaya ya kiomboi wilayani Iramba mkoani Singida
Mwenyekiti wa hamashauri ya wilaya ya Iramba Mhe: Simion Tyosera akiongea na wananchi siku ya kuadhimisha siku ya macho duniani katika hospitali ya wilaya ya kiomboi wilayani Iramba mkoani Singida
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl Linno Mwageni akiongea na wananchi siku ya kuadhimisha siku ya macho duniani katika hospitali ya wilaya ya kiomboi wilayani Iramba mkoani Singida
Baadhi ya wagonjwa wa macho baada ya kufanyiwa upasuaji wa Mtoto wa jicho ili kuwawezesha kuona tena katika siku ya maadhimisho ya macho duniani yaliyofanyika katika hospitali ya wilaya ya kiomboi wilayani Iramba mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt, Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, Kulia ni Mkurugenzi Mkazi shirika la Sightsavers Ndgu, Gozibert Katunzi na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula.
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi.
Katika kuadhimisha siku ya Macho Duniani, Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ameweka jiwe la ufunguzi kwenye jengo la kutolea huduma za macho hospitali ya wilaya Kiomboi wilayani Iramba leo tarehe 10.10.2019
Dkt Rehema Nchimbi ameshukuru sana shirika la Sightsavers kwa kushirikiana na Benki ya Standard Chartered kwa Mradi huu wa Afya ya Macho unao fahamika kwa jina la MAONO PROJECT.
“Niwashukuru sana shirika la Sightsavers kwa kushirikiana na Benki ya Standard Chartered ninawashukuru sana watalaam wote wa ngazi mbalimbali wanahusika na afya ya macho”.
Dkt Rehema Nchimbi aliongeza kusema “Kuona ni kuamini, tujiongeze na kuwavusha salama wakiwa na msingi ya macho, tusisubili mpaka tatizo limetokea, tuone ninamna gani tunavyoweza kujikinga kuwa na tatizo, na kinga ya msingi zaidi ni ile ambayo itaambatana na hatua zote za ujauzito na mpaka kuzaliwa kwa huyu mtoto na jinsi atavyolelewa.
Kauli mbiu yetu ya maadhimisho ya afya ya macho duniani ni KUONA NI KUAMINI na msisitizo ni kupima. Katika tafiti mbalimbali asilimia 80 ni upofu unaotibika, matatizo yanayohusiana na macho yanatibika, inawezekana kuna mahali tunachelewa kabla tatizo halijawa kubwa, tusifanye mchezo na macho yetu, tuache kuchukulia afya ya macho kwa jambo rahisi rahisi, nasisitiza umuhimu wa afya ya macho, ni kiungo muhimu kwenye mwili wa binadamu.
Macho haya yanakupa kuamini, na kuamini ni suala la msingi katika maendeleo, ni rahisi kuamini kila tunachoelekezwa kwa kuona. Macho yanatusaidia kutambua
Kuona ni kuamini Macho yanatusaidia sana katika kutenganisha, ukiona kitu ambacho sio chema, ni rahisi sana kutenganisha kizuri na kibaya, Macho ni ishara ya kujua yupi wa kuamini na yupi wa kutokuamini, macho yanakazi kubwa sana, kuona ni kuamini, tusifanye mzaa na afya ya macho. Hivi sasa serikali inafanya kazi kubwa sana chini ya Mhe Rais wetu Dkt John Pombe Joseph Magufuli, wengine macho yetu hayaoni Miradi mikubwa inayotekelezwa nchini, ujue afya yake ya macho inamatatizo, lazima kushughulika na afya yake ya macho.
Vile vile Dkt Nchimbi ameendesha harambee ya kuchangia huduma ya macho na kuchangia laki tano (500,000)
Shuhuli ya upimaji Macho bure na matibabu imefanyikia katika hospital ya wilaya ya Kiomboi wilayani Iramba mkoa wa Singida.
Ikiwa ni sehemu ya Serikali ya Tanzania kuungana na Mataifa mengine Ulimwenguni kuadhimisha siku ya huduma ya Afya ya macho.
Siku ya Afya ya Macho Duniani huadhimishwa duniani kote Alhamisi ya pili ya mwezi Oktoba ya kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha jitihada za kutokomeza upofu unaozuilika duniani. Maamuzi ya kuadhimisha Siku ya Afya ya Macho Duniani yalifikiwa na Lions Club International Foundation mnamo mwaka 1998, na baadae kuungwa mkono na wadau wengine wa Huduma za Macho ambao ni pamoja na Shirika la Afya Duniani, Muungano wa Mashirika ya Kimataifa yanayojihusisha na Huduma za Macho (International Agency for Prevention of Blindness), Serikali mbalimbali, wataalamu wa masuala ya afya, taasisi mbalimbali na watu binafsi kuwa, ni tukio mahususi la kuhamasisha utekelezaji wa Dira ya Kimataifa ya Kutokomeza Upofu Unaozuilika Duniani ifikapo mwaka 2020 kwa kuthamini Haki ya Kuona kwa wote (Vision 2020: The Right to Sight). Serikali ya Tanzania iliridhia na kuungana na Mataifa mengine duniani katika kutekeleza azimio hili mnamo tarehe 23 Mei 2003.
Matatizo makubwa yanayosababisha upofu unaoweza kuzuilika hapa nchini na dunia kwa ujumla ni:-
Akisoma taarifa, Mkurugenzi Mkazi Sightsavers Ndug. Gozibert Katunzi alisema shirika la Sightsavers lilianza kufanya kazi katika Mkoa wa Singida Mwezi Aprili 2016, kufikia leo tumesha kuwepo Mkoani kwako kwa kipindi cha miaka mitatu na miezi Mitano.
Shirika la Sightsavers limekuwa na Ushirikiano Mzuri sana kwa kipindi chote tulicho fanya kazi katika Mkoa huu. Tunashukuru sana kwa Ushirikiano Uliopo kuanzia ngazi za Chini (Kijiji hadi Mkoa)
Mradi huu wa Afya ya Macho unao fahamika kwa jina la MAONO PROJECT. Umefadhiliwa na shirika la Sightsavers kwa kushirikiana na Benki ya Standard Chartered
Ifahamike kuwa mradi huu unatekelezwa kwa kufuata miongozo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na vigezo vya shirika la Afya Duniani (WHO).
Tukiwa katika tukio hili la uzinduzi wa jengo la kutolea huduma za afya ya macho, ifahamike kuwa andiko la mradi lililenga kukarabati vyumba vinne katika hospitali ya wilaya za Manyoni, Iramba, Singida Vijijini na Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida na Sio Kujenga Jengo hili unalo lizindua siku ya leo.
Kila Wilaya ilipangiwa kiasi cha milioni arobaini na saba ili kukarabati vyumba vilivyo kuwa vina tumika kutolea huduma za Macho, kabla ya Mradi huu kuanza katika Mkoa wako.
Kutokana na Ubunifu na kujali kwa viongozi wetu wa wilaya hizi, Ofisi ya Mkurugenzi (DED), Mganga Mkuu wa Wilaya na Mwentekiti wa Halmashauri waliona kuwa kiasi hicho cha fedha kinatosha kujenga jengo hili.
Baada ya kukosa ramani toka Wizara husika za Serikali, Sightsavers kwa Kushirikana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya na Mganga Mkuu wa Mkoa,na Daktari Bingwa wa Macho tuliweza kuandaa Mchoro huu pamoja na makisio ya gharama ya ujenzi kwa kushirikiana na wahandisi wa wilaya na Mkoa. Hivyo kupata mchoro ulio tuletea jengo hili unalo zindua leo.
Isingekuwa ubunifu na utayari wa Viongozi katika Mkoa wako, tungekarabati chumba kimoja tu kilicho kuwepo katika Hospitali hii ya Wilaya.
Ndugu Mgeni Rasmi: Shirika la Afya Duniani (WHO), lina nguzo muhimu sita (Six building blocks). Mradi huu wa MAONO, umejikita katika kutekeleza Malengo ya Kitaifa na Kimataifa kwenye eneo hili ya Afya ya Macho, na Tumepata mafanikio makubwa tangu tuanze kufanya kazi katika Mkoa wako
Sensa ya Makazi na watu ya Mwaka 2012 inaonyesha kuwa Mkoa wa Singida una Jumla ya Wakazi 1,370,637. Kati ya hao Mradi huu umepanga kuwafikia Wakazi 296,200. Watu wazima 120,000 na Watoto wa shule za Msingi 176,200. Sawa na Asilimia 21.6% ya Wakazi wote kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Maeneo tuliyo fanya kazi tangu tuanze na Ushauri kwa Kila eneo
1. Utoaji wa Huduma za Afya ya macho (Eye health Service Delivery):
a) Mradi huu umepanga kufikia watu wazima laki moja na elfu ishirini kwa miaka minne (120,000) tumesha fikia watu 74,420 sawa na Asilimia 62.2 ya lengo la Mradi kufikia Juni 2020.
➢ Watu 56,604 wamepatiwa matibabu mbalimbali ya magonjwa ya macho
➢ 5,687 wamepata huduma ya upasuaji wa mtoto wa jicho na
➢ 5,061 wamepatiwa Miwani za kuona mbali na karibu
Kwa takwimu hizo inaonyesha kuwa jumla ya watu 67,362 walikutwa na matatizo ya macho kati ya 74,420 sawa na asilimia 90.5% (Hii inaonyesha kuwa wananchi hawajitokezi kupima hadi wasikie kuna kliniki tembezi au wakiwa tayari ni wagonjwa.
b) Kwa wanafunzi wa shule za Msingi tumesha fikia 141,227 kati ya 176,200 watakao fikiwa hadi Disemba 2019, sawa na asilimia 80% ya lengo la Mradi
Shirika la Afya Duniani WHO, linaelekeza kuwa kwa kila watu milioni moja (1,000, 000) macho 2,000 yanahitaji upasuaji wa mtoto wa jicho kila mwaka hivyo kwa Mkoa wako kila mwaka Zaidi ya macho 2,700 yanahitaji huduma ya upasuaji wa mtoto wa jicho.
Takwimu za mwaka 2015 kabla ya kuanza kwa Mradi huu zinaonyesha kuwa Mkoa ulifanya Upasuaji kwa watu 530 tu, kulinganisha na Mwaka
2018 ambapo Mkoa ulifikia Watu 2,600. Hii inaonyesha kuwa Mkoa huu unaweza kufikia lengo la Shirika la Afya Dunia kama utaendeleza kufuata mbinu zilizo tumika kutekeleza Mradi huu.
2. Kuboresha utoaji wa taarita za huduma za macho kutumia mifumo iliyopo: Mradi uliweza kutoa mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa za huduma za afya ya macho kwa wataalamu wanao toa huduma ya macho 16, pamoja na kuwapatia kompyuta mpakato (Laptop) waratibu wa macho wa wilaya zote pamoja na Mratibu wa Macho Mkoa). Mradi umekuwa ukifanya ufuatiliaji kila mwezi ili kuhakikisha taarifa zinazo kusanywa zina zingatia Vigezo vya Serikali na Mfumo wa MTUHA.
3. Rasilimali watu kwa ajili ya huduma za Afya ya Macho: Inafahamika kuwa Mkoa wa Singida una Daktari Bingwa wa Macho, na alikuwa sehemu ya kuandaa andiko la mradi huu mwaka 2015. Kabla ya kuanza kwa mradi mwaka 2015 Mkoa ulikuwa na watumishi wafuatao:
a. Wauguzi wa Macho (Manyoni Wawili (2), Iramba mmoja (1) Hospitali ya Mkoa mmoja (1) na Singida vijinini mmoja (1), Kupitia Mradi huu jumla ya Wauguzi Kumi na Sita (16), wamepatiwa mafunzo kutoka Chuo Afya ya Macho Mvumi b. Kulikuwa na Madaktari Wasaidizi Wawili (Singida Vijijini na Itigi, na wote hawakuwa Wanatoa huduma za Afya ya macho kutokana na Ukosefu wa Dawa na Vifaa tiba, Kupitia Mradi huu Tumeweza kufadhili mafunzo ya Miaka Miwili Katika Chuo Kikuu cha Afya KCMC kwa Madktari Wasaidizi Wanne (4) Manyoni, Iramba, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na Kituo ch Afya Sokoine. Hivyo;
4. Kuwezesha Upatikanaji wa dawa na Vifaa tiba. Mradi ulifanya kazi kwa karibu na Mkoa wako Kupitia Daktari Bingwa wa Macho Mkoa na kuainisha vifaa dawa mbalimbali na Vifaa vya kutolea huduma za lengwa kwa kipindi chote.
Shirika linaomba Mkoa wako uhakikishe vifaa hivyo vinatumika kuwapatia wananchi huduma bora za afya ya macho na sio vikae kwenye maboksi kama ilivyo onekana kwenye baadhi ya kliniki za kutolea huduma ya afya ya macho.
5. Fedha kwa Ajili ya huduma za Macho (Eye Health Financing) Taarifa ya Daktari Bingwa wa macho ya mwaka 2015, inaonyesha kuwa Mkoa ulipanga kiasi cha shilingi milioni sita tu (6,000,000/=) kwa ajili ya kutoa huduma za macho, Kiasi hicho kilipangwa na Hospitali ya Mkoa tu, Halmashauri zote hazikuwa zimeweka fedha kwa ajili ya huduma mbalimbali za macho. Watekelezaji wa Mradi huu kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Macho Mkoa wameweza kutoa huduma za upasuaji bure kwa wahitaji wengi, tangu kuanza kwa Mradi. Taarifa ya Daktari Bingwa wa macho inaonyesha kuwa gharama ya kufanya upasuaji wa jicho moja ni zaidi ya elfu sabini (70,000/=) hivyo bila Serikali kuwekeza fedha za kutosha Mkoa hautaweza kuendeleza huduma hizi za upasuaji wa mtoto wa jicho.
Shirika liliweza kufanya utafiti mdogo na kuandaa Mkakati wa Uendelevu wa Huduma hizi
Hivyo basi ili mkoa uweze kupata fedha za kuendeleza huduma hizi ni lazima watu wengi zaidi wajiunge na Bima ya Afya na wajitokeze kupima macho.
6. Kuboresha usimamizi wa huduma za Macho, Kupitia mradi huu kumekuwepo na vikao mbalimbali vya kila robo mwaka ili kuwaleta wadau muhimu kama, Wajumbe wa Kamati ya Afya Mkoa (RHMT), Wajumbe wa Kamati za Afya Wilaya (CHMTs) pamoja na Wataalamu wa Macho ili kujadili changamoto mbalimbali zinazo jitokeza. Mradi huu umeweza kuwezesha Wataalamu wa Afya ya Macho Mkoa, ili washiriki katika kuandaa Mpango Mkakati wa Afya ya Macho Taifa (National Eye Care Strategic Plan 2018/2022. Mafunzo kwa
Tupende kukuhakikishia kuwa Shirika la Sightsavers litaendelea kufanya kazi kwenye Mkoa wako, na tayari tumeweza kushirikiana na wataalamu wako (Daktari Bingwa wa Macho) kuandaa andiko lingine la mradi hivyo basi siku chache zijazo tutazindua Mradi wa Afya ya Macho Jumuishi – Utakaofadhiliwa na Serikali ya Uingereza Kupitia taasisi yake ya Misaada (UK-AID).
Tunapenda kutambua mchango wa wataalamu wako wa afya ya Macho ngazi zote; Na kipekee tunapenda kutambua Mchango wa Dktari Bingwa wa Macho Dr. Ng'hungu Lufunga Kuzenza na Mteknojia wa Macho Mkoa Ndugu. Dismas Kimvule kwa kuweza kushiriki katika kuandaa Maandiko Mbalimbali ili Mkoa uweze kuboresha huduma za Macho.
Wataalamu hao wameweza kuwakilisha Mradi huu vizuri ndani na nje ya Nchi hivyo kuletea sifa nyinigi Mkoa na Shirika la Sightsavers Tanzania kwa kipindi chote tulicho fanya kazi hapa.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.