Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata jimbo la Iramba Magharibi wamekula Kiapo Cha Kutunza Siri na kujitoa kwenye vyama vya siasa ili kuanza mafunzo rasmi kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Akifungua mafunzo hayo 04/08/2025 Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Iramba Magharibi Bi. Magreth Segu amewataka wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata kuzingatia na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zote za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unao tarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
"Ndugu zangu wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata nawasisitiza kusoma kwa umakini katiba, Sheria, Kanuni, Miongozo na Maelekezo mbalimbali yalioyotolewa na yatakayotolewa na Tume na ulizeni ili mpate kufafanuliwa kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine yatakuwa na changamoto za kufahamu ili kuwarahisishia katika utekekelezaji wenu wa kazi za Uchaguzi."
Mafunzo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata yatafanyika kwa Siku tatu (3) Kuanzia tarehe 04-06 Agosti 2025 katika Kituo cha Chuo cha bibilia kilichopo kata ya Old Kiomboi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.