• Malalamiko |
    • Kuhusu sisi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Maoni |
Iramba District Council
Iramba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amefunga kwa muda mgodi wa ‘sekenke namba moja

Posted on: December 14th, 2019

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amefunga kwa muda mgodi wa ‘sekenke namba moja’  uliopo wilaya ya Iramba mkoani hapa kama tahadhari kupisha uchunguzi wa kina na kitaalamu kubaini chanzo kilichosababisha kutitia ghafla kwa sehemu kubwa ya udongo eneo hilo na kusababisha taharuki kwa wananchi.

Akizungumza kupitia mkutano wa hadhara kwenye eneo hilo la tukio, Dkt. Nchimbi alisema tangu kutokea kwa tukio hilo lisilo la kawaida (juzi), kila alipojaribu kuhoji nini hasa kimesababisha eneo hilo kuzama, na kilichozama hapo ni udongo pekee au kuna watu wamefukiwa? Lakini mpaka sasa maelezo anayopokea ni kugongana-gongana.

 Alisema baadhi ya wamiliki wa maeneo hayo walimweleza kuwa kuzama (kutitia) huko kwa udongo kumesababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha. Wakifafanua kwamba maji ya mvua yalitiririka na kukutana na nyufa, na hatimaye kulainisha udongo uliokuwa umeshikana na nguzo, na kupelekea udongo kuachia na kutitia.

“Nikiwa Mkuu wa mkoa huu, tena mama ambaye ni lazima nisimame katika kuhakikisha usalama na mazingira mazuri ya kunufaika na haya ambayo Mwenyezi Mungu ametupa, kuanzia leo Disemba 12, 2019 ninapafunga hapa, ninafunga mgodi namba moja kupisha uchunguzi wa kina mpaka pale mtakapopewa taarifa,” alisema Nchimbi na kuongeza;

“Ninafunga namba moja ila namba mbili iendelee. Nafunga sekenke namba moja hadi pale wataalamu wa madini watakapokuja kufanya uchunguzi kubaini kama chanzo cha kutitia huko ni mvua kweli, na kama kuna madhara mengine ikiwemo vifo,”

Aidha, Nchimbi akitoa tathmini yake binafsi juu ya alichokibaini kwenye eneo la tukio, alisema kilichosababisha kutitia kwa udongo huo ni ubinafsi, ni tamaa, uroho wa kutaka kupata fedha kwa haraka, na watu kukosa hofu ya Mungu, huku akisisitiza kuwa watu wa aina hiyo ndio waliolipua zile nguzo zinazoshikilia pale kwa makusudi.

“Kuna nguzo pale tangu enzi za utawala wa Mjerumani zinazoshikilia, Mkoloni huyu pamoja na nguvu zake, pamoja na uwezo wake, na kwa kutambua eneo hilo la nguzo kuna dhahabu alisema endapo nitalipua hizi nguzo basi huu mgodi hautakuwepo, na hakuwahi kufanya hivyo,” alisema Nchimbi

Alisema anasubiri majibu ya wataalamu, ila sababu ya kwamba mvua imesababisha haimridhishi, kutokana na huko nyuma kuwapo na mvua nyingi zikiwemo za El-Nino lakini tukio kama hilo halikuwahi kutokea, huku akihoji kama ni mvua mbona sekenke namba 2 haijadhurika, mpaka sasa pako salama. 

Aliwataka wafanyakazi hao kuwa na subira kupisha uchunguzi ili kubaini kwa haraka kama ni mvua kweli, na kama sababu itakuwa ni mvua basi atalazimika pia kuufunga mgodi huo kusubiri mpaka pale msimu wa mvua utakapomalizika. Aidha alisema kama ikibainika atakuwa amesababisha mtu basi atatamani ikiwezekana afutiwe kabisa leseni ya kujishughulisha na madini.

Alisema mara kadhaa zinapotokea dhoruba kama hizo wanaokufa huwa ni wafanyakazi, huku wamiliki wa migodi na miduara hiyo wakiendelea kuwa salama. Alisema mathalani leo (juzi) alipokuwa akiongea na wamiliki hao aliwauliza kwanini msiwe mnatangulia kufa ninyi? Maana wanafanya upuuzi sababu wao hawaingii huko.

“Nataka niwahakikishie wafanyakazi Rais Magufuli anawapenda sana, na eneo hili lote mlimchagua kwa kura nyingi, fursa hii ya madini haikutolewa na serikali au kuruhusiwa ili watu wafe hapana! Tunataka madini yetu yasigeuke chanzo cha huzuni na maafa, bali yatuletee amani, furaha, maisha marefu kwa vizazi na vizazi…na hii ndiyo furaha ya taifa lolote lile ambalo linajipenda,” alisema Dk Nchimbi

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba ambaye eneo hilo ni sehemu ya jimbo lake, aliomba wananchi watoe ushirikiano wakati wote zoezi la ukaguzi litakapokuwa likiendelea, na kuwataka kuchukua tahadhari kuepuka athari nyingine inayoweza kujitokeza hata wakati wa uokoaji.

“Pia ninaomba tupewe ruhusa kwa wale wenye mitambo yao hapo nje na wana mawe ambayo tayari wamekwisha yachimba basi waendelee kusafisha wakati taratibu nyingine zikiendelea…tupewe ruhusa ya kusafisha na sio kuchimba,” alisema Nchemba

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA November 03, 2023
  • KUITWA KAZINI November 29, 2023
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2018 HALMASHAURI YA WILAYA IRAMBA January 05, 2019
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2018 January 05, 2019
  • Angalia Zaidi

Habari mpya

  • Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wamefanya ziara ya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa Wilayani Iramba

    October 24, 2023
  • RAIS DKT. SAMIA AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI SINGIDA KWA KISHINDO, WANANCHI WAMSHUKURU KWA MIRADI YA MAENDELEO

    October 17, 2023
  • MKUU wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amepokea rasmi Mbio za Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani Tabora na aliyekabidhi ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Batlida Briani.

    September 22, 2023
  • MKIMBIZA Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaibu Kaim amewataka Watanzania kuhakikisha wanakemea vitendo vya rushwa kwa maelezo kuwa rushwa inakwamisha maendeleo ya Mkoa pamoja na Taifa kwa ujumla

    September 22, 2023
  • Angalia Zaidi

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
Video Zaidi

Linki za Haraka

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Linki Zinazohusiana

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Kuhusu sisi

    KIOMBOI, IRAMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Simu: 026 - 2532253

    Simu: 026 - 2533001

    Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • FAQ
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.