By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amemuagiza kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Marietha Kasongo kupita kila kibanda na kumsainisha mkataba atakayekutwa humo.
Luhahula ameyasema hayo leo Jumamosi Novemba 9, 2019 wakati akiongea na wafanyabiashara wa vibanda vya stendi na sokoni kiomboi wilayani Iramba Mkoa wa Singida Tanzania.
Akijibu kero ya stakabadhi zilizotolewa kwa wafanya biashara ambao wakienda kwenye mfumo wa halmashauri hazimo, Luhahula ameelekeza takukuru kuchunguza na kutoa taarifa kwenye kamati ya ulinzi na usalama
“Nimeelekeza takukuru wachunguze mara moja ili watuletee taarifa kwenye kikao cha kamati ya ulinzi na usalama kinachokuja,” amesema
Amewaambia watu wa Iramba kufanya kazi kwa sababu suala la vibanda wafanyabiashara hao walikaa na Mkuu huyo kwenye ofisi yake na kukubaliana kulipa 20,000 kwa mwezi, baadae maamuzi hayo yalipitishwa na kamati ya fedha ya Halmashauri hiyo.
Akipongeza hatua iliyochukuliwa ya kukutana na wafanyabiashara hao Mkuu wa Wilaya hiyo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Samwel Shila amesema katika dunia ya leo kupanga ni kuchagua kuishi maisha gani, kuwa yeye na wantendaji watajifungia katika vikao na watoke na maamuzi ya kumsainisha mkataba aliyoko kwenye kibanda.
Shila amebainisha kuwa hawawezi kukubali kuona watu wanao tengeneza mambo kuharibu mabadiliko ya kiomboi huku akiwataka wao ndio wajitenge.
“ Kuna watu hapa wanataka kuwatumia kupita kwenye kinvuli cha wafanyabiashara ili iwe ndio kama kero ya watu wote, haiwezekani,” amesema
Akiwaeleza wafanyabiashara hao Makamu Mwenyeketi wa Halmashauri hiyo, kuwa watapita kwenye kila kibanda hata kama kitakuwa kimefungwa kitafunguliwa na kutafuta mtu mwingine wampangishe na atakaye uliza watakutana mahakamani ikiwa ni njia ya kutatua mgogoro huo.
Akiongea katika kikao hicho Mwanasheria wa Halmashuri hiyo Gerald Samwel amesema kuwa vibanda ni mali ya Halmashauri na kuwa wajenzi waliopangishwa kwa sheria ya ardhi 1999 hairuhusiwi kumpangisha mtu mwingine bila ruhusa ya mwenyenyumba (Halmashauri).
“ Sisi hatujakuruhusu ni lazima uombe kibali kwa maandishi na uruhusiwe kwa maandishi, tutarudi tena tutakayemkuta ndio tutasaini naye mkataba,” amesema
Awali akitoa kero yake mmoja wa wajenzi wa vibanda hivyo, Christina Juma amesema kama mtu yupo anayelipa 80,000 kwenye kibanda chake hiyo ni siri ya mwenyekibanda na mpangaji huku akibainisha kuwa mzunguko wa fedha unakuwa na ugumu kidogo na kuomba wapunguziwe kodi.
Naye Jumanne Mkumbo mmoja wa wapangaji wa vibanda hivyo ameilalamikia Halmashauri kupata mpangaji ambaye atakuwa ni mmiliki halali ambaye watakuwa wanapanga kwake moja kwa moja ili kuondoa usumbufu wa kupandishiwa kodi, kupanga mara mbili na kulipa kwa mjenzi na Halmashauri.
Kwa upande wake katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, Ibrahim Mjanaheri amempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kuwa msikivu kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati.
“ Sisi kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya tunafarijika na kufurahi sana kufanya kazi na Mkuu wa Wilaya ambaye ni Msikivu” amesema Mjanaheri
Afisa Biashara wa Wilaya ya Iramba, Prospa Banzi akijibu maswali mbalimbali ya wafanyabiashara wa Mji wa Kiomboi Wilayani Iramba wakati wa kikao cha Mkuu wa Wilaya na wafanyabiashara kilichofanyika ukimbi wa halmashuri kulia kwake ni Muandishi wa vikao vya Halmashauri, Shiwariael Malunda na kushoto kwake ni mwanasheria wa Halmashauri Gerald Samwel. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba wakifuatilia kwa makini kikao cha Mkuu wa Wilaya Emmanuel Luhahula na wafanyabiashara wa kiomboi ukumbi wa halmashauri. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya wafanyabiashara wa kiomboi wakifuatilia kwa makini kikao cha Mkuu wa Wilaya Emmanuel Luhahula na wafanyabiashara wa kiomboi ukumbi wa halmashauri. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.