Ofisiya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba na Viongozi wa Kata ya Tulya wamefanya ukaguzi wa kushutukiza katika ziwa Kitangiri kata ya Tulya leo 24.09.2018
Katika ukaguzi huo wamebaini Nyavu haramu nne(4) aina ya makokoro zenye jumla ya urefu wa yadi 1900, sawa na futi 5700 na thamani ya Tshs 2,800,000, zimeteketezwa kwa motombele ya Mkutano wa hadhara wa kijiji najamii ya wavuvi kutoka kijiji cha Doromoni, kata ya Tulya, wilayani Iramba.
Nyavuhizo haramu zilikamatwa katika Doria iliyofanyika katika ziwa Kitangiri eneo lakambi ya uvuvi ya Usiulize iliyoko upande wa Wilaya ya Meatu, ikishirikisha Kikundi shirikishi cha ulinzi wa ziwa (BMU) Tarehe 19/09/2018 na watuhumiwa kufanikiwa kutoroka na kuterekeza nyavu hizo.
Zoezi hili limefanyika kama utekelezaji wa Sheria ya uvuvi na 22 ya mwaka 2003, Tamko la Mhe. Rais alilolitoa juu ya kuthibiti matumizi ya makokoro, mpango mkakati wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba kuthibiti matumizi ya zana haramu katika shughuli za uvuvi ziwa kitangiri.
Msimamizi wa sekta ya Uvuvi (W) Ndg. Deogratius K. Isagala, aliongeza kusema Mfumo wa uteketezaji wa makokoro mbele ya mikutano ya hadhara,wananchi na jamii ya wavuvi mara baada ya wahusika kutoroka na makokoro yanapokuwa yamekamatwa ni mkakati wa kutoa somo juu ya kupiga vita matumizi ya Zana haramu za uvuvi wa makokoro katika Ziwa Kitangiri, kuonesha hasara inayoweza kuwapata wavuvi haramu pindi makokoro yanapokuwa yamekamatwa,hivyo kuwa ni njia ya kisaikolojia yakuwakatisha tamaa wavuvi haramu na njia halisi ya kupunguza idadi ya zana haramu za uvuvi. Uteketezaji wa nyavu hizo hadharani licha ya kujenga imani miongoni mwa jamii ya wavuvi halali, unathibiti mzunguko haramu wa nyavu haramu zilizokamatwa kurudishwa tena ziwani kwa watendaji wasio waaminifu.
Aidha Baadhi ya athari ya matumizi ya makokoro katika Ziwa Kitangiri ni pamoja na kuvua samaki wadogo wenye ukubwa chini ya inchi 3’ utakaoshusha ubora wa samaki na bei ya soko, uvuvi wa samaki wadogo(parent stock) ambao ni wazazi wa kesho hivvo kunaweza kupunguza kiwango cha uzalishaji wa samaki wa kesho katika ziwa, Kuharibu mayai ya samaki, uvuvi wa makokoro kwa njia ya kuvuta(kukokora) mara kwa mara kunaharibu sakafu ya ziwa,kuharibu uoto wa asili ndani ya Ziwa na makazi ya viumbe hai kama vile samaki, wanyama aina ya viboko na mimea iliyomo ndani ya ziwa.
Diwaniwa kata ya Tulya Mhe. Wilfred Kizanga (CCM) amesema Kiwango kidogo cha uzalishaji wa samaki na ubora unawafanya na wavuvi kutumia nguvu na muda mwingi kuvua samaki wachache na wenye bei ndogo ya soko kutokana na matumizi ya muda mrefu ya zana haramu za uvuvi, lakini pale mikakati ya matumizi ya zana halali itakapofanikiwa na kuzaa matunda kwa asilimia 100% wavuvi watatumia muda mfupi kuvua samaki wengi wenye ubora na bei nzuri ya soko.
Aliongeza kusema zoezi hili endelevu limelenga kuhakikisha kuwa Ziwa kitangiri linaendelea kuwa ni moja ya rasilimali muhimu,iliyopo katika Wilaya ya Iramba, shughuli mbalimbali za uvuvi zinazofanyika katika Ziwa hili zitaendelea kuborekana kutoa mchango mkubwa katika kuboresha lishe ya jamii na kukuza uchumi wa kipato cha kaya, kuboresha maisha na maendeleo ya wananchi wa Iramba, Igunga, Kishapu na Meatu na watanzania wote kwa ujumla na hatimaye kufikia kiwango cha uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.