Watoto wilayani Iramba wakisherekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kijjiji cha Nguvumali kata ya Ndago tarafa ya Ndago wilaya ya Iramba leo Tarehe 16.06.2019.
Mgeni rasmi akitembelea kikundi cha wajasiliamali kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kijjiji cha Nguvumali kata ya Ndago tarafa ya Ndago wilaya ya Iramba leo Tarehe 16.06.2019.
Muwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Iramba Ndg. Dijovison Ntangeki akizungumza na wananchi wa Ndago kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kijjiji cha Nguvumali kata ya Ndago tarafa ya Ndago wilaya ya Iramba leo Tarehe 16.06.2019.
Muwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Iramba Ndg. Dijovison Ntangeki ameungana na wananchi wa Iramba kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yamefanyika kijjiji cha Nguvumali kata ya Ndago tarafa ya Ndago wilaya ya Iramba leo Tarehe 16.06.2019.
Akizungumuza na wananchi wa Ndago Ndg. Ntangeki alisema “Ninayo furaha kubwa kunialika kuwa mgeni rasmi katika siku hii ya mtoto wa Afrika. Ni utamaduni wetu kila mwaka kukutana Tarehe kama ya leo na kukumbushana mambo ya msingi ambayo tunatakiwa kuyafanya kwa manufaa ya watoto wetu. Ni wajibu wetu sisi wazazi pamoja na walezi kuwarithisha watoto mila, desturi, tabia na mienendo mizuri kwa kuwa ndiyo wazazi wa kesho.
Kauli mbiu ya maadhimisho haya ya siku ya mtoto wa Afrika inaeleza kwamba mtoto ni msingi wa taifa endelevu, tumtunze, tumlinde na kumuendeleza. mtoto ni mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane. Tafsiri hii imetokana na mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto, mkataba wa Afrika kuhuhu haki na ustawi wa mtoto, sera ya maendeleo ya mtoto na sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009. Katika umri huu mtoto anahitaji malezi bora ili kuishi vizuri, kushirikishwa, kulindwa na kuendelezwa kiakili kwa ajili ya maisha yake ya baadaye ya utu uzima alisema Ntangeki
Siku ya mtoto wa Afrika ilitokana na wanafunzi kutoka mji wa SOWETO Afrika Kusini kuandamana wakidai mazingira bora ya kufundishiwa na kupatiwa elimu bora Tarehe 16 Juni 1976. Pia wakiomba kati ya mambo mengine kufundishwa katika lugha ya Kiafrikana. Matokeo yake wanafunzi wengi waliuwawa katika maandamano hayo ya Amani na utawala wa kibaguzi. Kuanzia mwaka 1991 siku ya mtoto wa Afrika imekuwa ikiazimishwa kama sehemu ya kukumbuka ya mauaji ya watoto hao wasio kuwa na hatia yaliyofanywa huko Afrika Kusini. Na mara nyingi ktika maadhimisho haya yanakuwa na kauli mbiu zenye lengo la kuhahakikisha mtoto wa Afrika anaendelea kulindwa na kuendelezwa katka Nyanja mbalimbali.
Aliongeza kusema “Watoto wanahaki za kipekee kwa sababu umri wao ni mdogo na hali ya utegemezi vinaweza kuwafanya wadhulumiwe na kutendewa vitendo vibaya. watoto wote wanahaki sawa bila kujali jinsi, rangi, kabila dini hadhi au hali ya afya. Umoja wa mataifa, serikali wazazi/walezi na jamii kwa ujumla wana wajibu wa kuhakikisha watoto wanapatiwa haki zao. Haki za watoto ni pamoja na:-
Haki ya kuishi inahusu kulinda na kuendeleza uhai wa watoto ikiwa ni pamoja na kuzuia magonjwa na kupat huduma za matibabu, chanjo na kufuatilia kukuaji, lishe bora, mavazi yanayositiri, makazi salama na maji safi na salama.
Haki ya kuendelezwa inahusisha maendeleo ya mtoto kiakili ikiwa ni pamoja na kupatiwa Elimu, tamaduni, mila, na desturi sahihi za jamii yake na vipaji vya watoto.
Haki ya kulindwa kuhakikisha mtoto analindwa dhidi ya unyanyaswaji na ubaguzi, ukatili (kimwili, kingono na kihisia) kumlinda dhidi ya unyonywaji ikiwa ni pamoja na ajira za utotoni, ndoa za utotoni, ukatili wa kijinsia na kumlinda dhidi ya mazingira hatarishi.
Haki ya kushiriki mtoto anapaswa kushirikishwa katika ngazi zote kuanzia kwenye familia, jamii na taifa.
Alisema Mzazi/mlezi anawajibu wa kuhakikisha anakuza kipato na uzalishaji ili aweze kuhudumia familia yake. Kuhakikisha familia inapata mahitaji yote ya msingi ili kukabiliana na madhara kipindi cha majanga. Familia ikiwa na kipato duni inamtumia mtoto au watoto wa kike kama sehemu ya familia kujipatia kipato. Kila famila lazima iboreshe uchumi wa kaya yake ili kuweza kuwaendeleza, kuwalinda na kuwatunza watoto na kuvunja mzunguko wa umaskini. Tafiti nyingi zinaonesha uchumi duni ndani ya familia ni moja wapo ya sababu ya mtoto kukimbia familia.
Elimu ni haki ya kila mtoto bila kujali hadhi, hali ya afya kama ulemavu, jinsia, rangi au kabila. Wazazi/walezi wanawajibika kwa kuhakikisha watoto wa kike na wakiume wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa shule. Mzazi/mlezi anawajibu wa kuhakikisha na kufuatilia kuwa mtoto anasoma na maendeleo yake yanakuwa ni mazuri na anapatiwa mahitaji yote ya kielimu. Jamii kwa ujumla inawajibu wa kuhakikisha mazingira ya kujifunza ni bora na wanachangia katika Upatikanaji wa chakula shuleni.
Jamii pia inawajibu wa kushiriki katika uendeshaji wa shule na kushiriki na watoto wao katika shughuli mbalimbali za kielimu. Walimu, wazazi na walezi wana wajibu wa kufuatilia na kuhakikisha watoto wote wa kike na kiume wanalindwa na vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia wakati wa masomo.
Lishe bora kwa mtoto ni sehemu ya mahitaji muhimu ili kuweza kumendeleza mtoto. Pia malazi na makazi bora kwa mtoto ni jambo la msingi la kumfanya mtoto aweze kulelewa katika mazingira safi na salama. Suala la kumpatia mtoto malazi na makazi bora ni kumjengea mtoto maendeleo ya kifikra na kisaikolojia. Mzazi akiboresha lishe, malazi na makazi ya familia ni sehemu ya mkakati wa kumtunza, kumlinda na kumuendeleza mtoto.
Familia ina wajibu wa kutunza chakula cha kutosha kwa manufaa ya mtoto. Ndugu wananchi ili kuweza kustawisha familia ni budi kila mwananchi kuhakikisha anakuwa na chakula cha kutosha kwa ajili wa wana kaya wote wakiwemo watoto. Kaya isipokuwa na chakula husababisha familia kuvunjika kwani watoto hukimbia kaya kwenda kutafuta chakula Mahali popote bila kujali mazingira kama ni salama au hatarishi. Njaa ya mara kwa mara ndani ya kaya ni kikwazo kwa maendeleo endelevu na uimarishaji wa fursa kwa watoto. Jukumu la kuhakikisha chakula kinapatikana kwa watoto ni jukumu la msingi la wazazi au walezi.
Malezi ni mchakato wa maelekezo, ushauri na mafundisho kwa mtoto yanayosaidia kumkuza mtoto kimwili, kihisia, kimaarifa na kumwelekeza kimazingira kuanzia mtoto anapozaliwa hadi kuwa mtu mzima. Ndugu wananchi ili taifa liweze kupiga hatua ya maendeleo ni lazima Kufundisha watoto maadili yaliyo mema. Maadili ni pamoja na hehima, utii kwa watu wote bila kujali hadhi zao, kuelimisha watoto kuchukia vitendo vya kuomba omba kuchukia Rushwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kujituma na kufukia malengo yao. Kama familia zitazingatia maadili yaliyo mema zitakuwa zimetoa mchango mkubwa wa kuimarisha ulinzi na fursa kwa watoto wote.
Kushirikiana na serikali na Wadau wengine katika kuhakikisha huduma zinapatikana kwa viwango stahiki katika maeneo yao. Ili mtoto aweze kulindwa vyema huduma mbalimbali za jamii zinatakiwa kupatikana. Huduma kama vile Elimu inahitaji miundo mbinu pamoja na rasilimali watu, huduma ya afya na maji vilevile. Ni wajibu wetu wazazi/ walezi kwa kushirikiana na serikali kuboresha mazingira ya kutolea huduma mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kumlinda, kumtunza na kumuendeleza mtoto. Juhudi hizo ni pamoja na kujenga hostel za watoto, kujenga zahanati pamoja na kushiriki kikamilifu katika kuimarisha juhudi za Upatikanaji wa maji safi na salama kwa kaya.
Ili kuitikia wito wa kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika 2019 kila mwananchi anapaswa kutoa taarifa kwa matendo au vitendo vinavyoathiri maendeleo ya mtoto hasa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya mtoto. Taarifa hizo zinaweza kutolewa kwa Viongozi wa serikali wa eneo husika (afisa Mtendaji wa kijiji au kata), timu za ulinzi na usalama wa watoto ana afisa wa ustawi wa jamii/ maendeleo ya jamii, polisi (dawati la jinsia na watoto), kituo cha afya, mashirika yanayotetea haki za watoto mfano world vision, mashirika yanayota msaada wa kisheria.
Serikali imeedelea kuboresha huduma za afya kumtunza, kumlinda na kumendeleza mtoto. Kupitia sera ya afya inatambua kuwa kundi la watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wana haki ya kupata huduma za afya bure. Katika Halmashauri ya wilaya ya Iramba ina Jumla ya watoto 43712 chini ya umri wa miaka mitano ikiwa kwa kiume 21967 na wakike 21715, wanaopata huduma za afya bila malipo zikigharimiwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe: Dkt John Joseph Pombe Magufuli Rais wa serikali ya awamu ya tano. Serikali inaendelea kuhamasisha na kuelimisha jamii kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) lengo likiwa ni kuweza kuwakinga watoto na magonjwa ambayo yanaweza kuathiri maendeleo yao kimwili, kisaikolojia na kiafya. Suala la kuwa na bima ya afya ni sehemu ya mkakati wa kitaifa ya kumtunza kumlinda na kuendeleza mtoto kwani pia mtoto ni sehemu ya familia
Katika kuhakikisha suala zima la kumlinda mtoto kupitia Idara ya afya, chanjo mbalimbali zinazozuia magonjwa zinatolewa na zinaendelea kutolewa kwa watoto. Ujenzi wa zahanati kila kijiji na kituo cha afya kila kata ni mwendelezo wa kuhakikisha kuwa mtoto wananweza kufikia huduma za afya pindi zinapohitajika. Hivyo nitumie nafasi hii kuwahimiza wananchi kufanya mambo yafuatayo.
Kaya ambazo bado hazijajiunga na CHF nazielekeza kuijiunga na CHF iliyoboreshwa kwa ajili ya manufaa ya mtoto na familia kwa ujumla
Kuwapeleka watoto kupata chanjo kadri ya maelekezo ya watoa huduma za afya
kutoa Elimu bila malipo kwa watoto wote kuanzia Elimu ya awali hadi kidato cha nne ni mkakati mwingine wa serikali wa kumuendeleza mtoto. Lengo la serikali ni kuhakikisha kila mtoto anapata Elimu kwani Elimu ni mlinzi wa kupambana na hadhara yanayoweza kuwakabili watoto. Wilaya ya Iramba ina Jumla ya watoto walioandikishwa Elimu ya awali mwaka 2019 ikiwa KE 4,928 na ME 5188 watoto walioandikishwa darasa la kwanza 2019 jumla ni watoto 8929 kati yao KE 4392 na ME 4537 waliohitimu Elimu ya msingi mwaka 2018 jumla ni watoto 3727 ikiwa KE 1961 na ME 1766 vilevile watoto walifaulu kuingia kidato cha kwanza 2019 ni Jumla ya watoto 3518 ikiwa KE 1861 na ME 1657 bado juhudi zinaendelea kuchukuliwa na serikali kuhakikisha kuwa mabweni kwa wananfunzi wa kike yanajengwa ili watoto wa kike waweze kulindwa dhidi ya madhara ambayo yanaweza kupunguza idadi ya watoto wa kike kupata haki ya Elimu.
Katika suala la Elimu naendelea kuhimiza wananchi kuchangia harakati za ujenzi wa mabweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum.
Jamii kuwa na mpango endelevu itayosaidia wanafunzi wote kupata chakula cha mchana shuleni ili kuongeza mahudhurio na ufaulu kwa ngazi zote.
Kuandikisha watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na kupatiwa cheti cha kuzaliwa bila malipo, serikali imendelea kutoa huduma mbali mbali kwa watoto hasa kundi la umri chini ya miaka mitano. Watoto chini ya umri wa miaka mitano katika wilaya yetu wameandikishwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa bila malipo. Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka muhimu ya awali kwa utambulisho wa mtoto. Zaidi ya watoto 38170 wamesajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa bila malipo. Napenda kusisitiza na kuelekeza wazazi au walezi wanaoishi na watoto ambao wako chini ya umri wa miaka 5 kuwapeleka kuandikishwa na hatimaye waweze kupatiwa vyeti vya kuzaliwa baada ya kutimiza vigezo vya kuandkishwa. Aidha vituo vya kuandikishwa na kutoa vyeti ni ofisi za maafisa watendaji wa kata pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoko katika kata husika. Watoto wa umri wa miaka mitano na kuenedelea waandikishwe na kupata vyeti vya kuzaliwa.
Serikali imeendelea kujenga miundo mbinu ya maji kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao. Vijiji mbalimbali vinamiundo mbinu ya maji, yote yanafanyika yakiwa na lengo la kusaidia kaya kupata huduma ya maji na kwa kuwa mtoto ni sehemu ya familia itasidia kumlinda na kumuendeleza.
Serikali imeendelea na mikakati mbalimbali ikiwemo mpango wa kunusuru kaya masikini. Mpango huu umelenga kupunguza umaskini ndani ya kaya hasa kumwendeleza mtoto amabaye ni taifa la leo na kesho. Halmashauri ya Iramba ina kaya Zaidi ya 5000 ambazo zimeandikishwa chini ya mpango wa kunusuru kaya maskini. Kaya hizi hupokea ruzuku ikiwa ni jitihada za serikali kuhakikisha inawalinda, kuwatunza na kuwaendeleza watoto walio katika kaya hizo. Nitumie nafasi hii pia kuwakumbusha wazazi na walezi ambao wako katika mpango huu kutumia fedha hizo kwa usahihi kwa kadri ya maelekezo ya mpango
Ndg. Ntangeki alisistiza
Familia kutunza chakula cha kutosha kwa manufaa ya mtoto pia jamii inatakiwa kuhakikisha inachangia chakula cha mchana shuleni,
Kuhakikisha kuwa jamii inaweka mikakati ya kumlinda, kumtunza na kumuendeleza mtoto,
Familia kuendelea kuzingatia malezi bora kwa mtoto, Kupeleka watoto chini ya umri wa miaka mitano cliniki,
Watoto kuandkishwa shule ya awali kwa kadri ya maelekezo ya watalaam wa Elimu
Wazazi kuendelea kupeleka watoto chini ya umri wa miaka mitano ili waandikishwe na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.
Kaya au familia kuendelea kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) iliyoboreshwa
Watoto kuendelea kutii na kuheshimu wazazi/walezi wenu
Wananchi kuenedelea kujikinga na ukimwi kwani bado hakuna tiba wala chanjo ya ugonjwa
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.