Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akipokelewa na viongozi mbalimbali wa chama, dini na Serikali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya maadhimisho ya uzinduzi wa kampeni ya wiki ya chanjo kimkoa yaliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Sehemu ya wanafunzi wa shule za msingi waliojitokeza kushuhudi sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kushuhudi sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni akizungumza wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Mratibu wa chajo mkoa wa Singida, Bi. Jadil Mhanginonya akitoa taarifa ya hali ya chanjo kwa mkoa wa Singida wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mheshimiwa Emmanueli Luhahula akizungumza wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kisemeo) akizungumza na kuwapongeza wananchi wenye umri wa miaka 55, wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Wananchi wenye umri wa miaka 55 wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani), wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi pamoja na viongozi wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wenye umri wa miaka 55, wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa sambamba na kikundi cha burudani, wakati wa sherehe za miaka 55 ya Muungano ambapo mkoani Singida ilifana kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chanjo, iliyofanyika Ndago katika halmashauri ya wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
MKOA wa Singida umeadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania kwa kuzindua kampeni ya wiki ya chajo mbalimbali ikiwemo ya polio ilikumkinga mtoto dhidi ya maradhi ambayo yanazuilika kwa chajo. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. RehemaNchimbi, amewataka wananchi kuendelea kuuenzi Muungano kwa kuwa umeendelea kudumisha mshikamano na undugu baina ya Watanzania wa bara na wa Zanzibar. “Sisisote wakazi wa mkoa wa Singida wajibu wetu ni kuendelea kuuenzi na kuulinda Muungano huu muhimu kwa maendeleo yetu, Tuutumie vizuri kwa kuhakikisha tunanufaika na fursa mbalimbali ikiwemo ya uchumi zilizopo ndani ya muungano ili kujiletea maendeleo katika mikoa na Tanzania kwa ujumla”.alisema Dkt. Nchimbi.
Akizungumza na wananchi wa ndago kuhusu kupanua wigo wa chanjo Dkt. Nchimbi amesema “watoto wanaeendelea kuzaliwa nje ya vituo vya kutolea huduma hali inayosababisha kukosa baadhi ya huduma za awali za chanjo. Mkoa unasisitiza kuwa uzazi salama uzingatiwe, wazazi wajiandae na kufuata ushauri unaotolewa kliniki wakati wakiwa wajawazito ili kuwa katika mikono salama wakati wa kujifungua. Hata hivyo, watoto wote wanapaswa kufikishwa kwenye vituo vya kutolea huduma ndani ya siku 14 za kuzaliwa ili wapatiwe chanjo hizo bila kujali wamezaliwa nyumbani au kwenye vituo vya kutolea huduma”.
Ameongeza kusema virusi vinavyosababisha saratani ya shingo ya uzazi (HPV), viepukwe ili kuwaepusha wanawake wengi na saratani ya shingo ya uzazi nchini humo ikiwemo ndoa za utotoni, kuwa na wapenzi wengi wa kushiriki nao ngono, magonjwa ya zinaa ikiwemo HIV, Matumizi ya bidhaa za tumbaku, ukosefu wa vitamin na maambukizi ya virusi vya HPV. “Siyo wanawake wote wanaogundulika kuwa na dalili hizi za awali wanafuata maelekezo na kurejea kupata matibabu ambayo ni muhimu sana ili kuzuia ugonjwa kuenea. Nichukue nafasi hii kuwakumbusha wananwake wote ambao hawawezi kufikiwa na chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kuwa, kufika kupata uchunguzi na matibabu ni njia pekee ya kuzuia ugonjwa huu kabla haujaleta madhara makubwa mwilini. Ugonjwa ukiachwa uenee inakuwa vigumu kutibiwa na kupona. Nitoe rai kwa jamii pia kuhakikisha mabinti zetu wanapata kinga kamili kwa kumalizia sindano zote 2 ili wasipate hizi changamoto ambazo wanawake wengi wanakumbana nazo na wengine kupoteza maisha.
Hata hivyo, chanjo hii haizuii magonjwa mengine kam virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa, mimba za utotoni na madhara yote yanayotokana na kuanza ngono katika umri mdogo. Hivyo maadili na tahadhali ziendelee kuzingatiwa kwa ajili ya usalama wao dhidi ya hatari hizi nyingine
Udhibiti wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ni makubwa sana katika mkoa wetu na taifa kwa ujumla. Mgonjwa wa mwisho kuugua ugonjwa wa polio nchini Tanzania ilikuwa mwaka 1996. mgonjwa huyu aligundulika huko katika mkoa wa mtwara
Hata hivyo mafanikio haya yawe chachu kwetu kuongeza juhudi katika kutumia huduma za chanjo kwani kweli zinafanya kazi. Chanjo hutoa kinga kwa wale tu wanaopata huduma na kukamilisha ratiba” alisema Dkt. Nchimbi.
ugonjwa wa malaria hauna chanjo inayotolewa katika nchi yetu. Ni ugonjwa hatari sana. Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha malaria katika mkoa wetu ni aslimia 2.3 lazima tupapambane kutokomeza ugonjwa huu kwa kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kuondoa mazalia ya mbu na kutumia vyandarua kwa usahihi. Tunahitaji kufikia hatua ambayo hakuna mwananchi anayeugua ugonjwa huu.
serikali yetu inaendelea kuwakinga watoto kwa kuwaptia vyandarua bure kila wanapotimiza umri wa miezi 9. Akina mama wajawazito pia kupatiwa vyandarua hivi bure kila wanapofika katika hudhurio la kwanza kwa ajili ya kumlinda mama na mtoto wake aliyetumboni
Wananchi jitokeze kupata vyandarua hivi na pia Halmashauri zote ziweke mazingira rafiki ya kupata vyandarua katika maeneo yote ya huduma ikiwemo vituo binafsi alisisitiza Dkt. Nchimbi.
Aidha Dkt. Nchimbi amewataadhalisha wananchi wote juu ya uwepo wa ugonjwa wa dengue katika mkoa wetu wa Singida ambapo tayari mgonjwa mmoja amegundulika kuugua ugonjwa huo baada ya vipimo vilivyopelekea maabara ya taifa kuthibitisha uwepo wa vijidudu vya ugonjwa huo. “Ugonjwa huo nao unaenezwa na mbu aina ya Aedes. Mbu huyu anapendelea kuuma mchana ambapo hujificha kwenye maeneo ya kivuli. Ni rahisi kumtambua mbu huyu kwani ni tofauti na mbu wngine. Mbu huyu ana mabaka meusi na meupe katika mwili wake.
Dalili za ugonjwa wa dengue pamoja na homa kali, vipele, maumivu, ya viungo na pia mgonjwa anaweza kuanza kutokwa damu mwilini kama vile puani, kwenye fizi na maeneo mengine mwilini. Kwa dalili hizi mgonjwa anaweza kudhaniwa ni ugonjwa wa malaria, surua au mafua. Nawasihi wananchi kuacha kufanya vipimo kwa macho na wala usikae na mgonjwa mwenye dalili hizi, mgonjwa afikishwe kwenye vituo vya kutolea huduma haraka alisistiza Dkt. Nchimbi.
Akisoma taarifa ya ya utekelezaji wa shughuli za chanjo kwa niamba ya katibu tawala mkoa wa Singida, Bi:Jadili Mhanginonya (RIVO) amesema mkoa wa Singida una Jumla ya vituo 203 vinatoa huduma za chanjo kwa mama wajawazito na watoto. Hili ni ongezeko la vituo 19 kutoka vituo 184 vilivyokuwa vinatoa huduma hiyo mwaka 2014.
Katika kipindi cha mwaka 2019, mkoa unatarajia kupokea Jumla ya majokofu 92 kutoka mpango wa taifa wa chanjo, majokofu ambayo yatasambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma na kuwafikia wananchi maeneo mengi zaidi. Majokofu hayo yanayotolewa kwa awamu baadhi (majokofu 14) yameshapokelewa na kusambazwa katika Halmashauri ya wilaya ya Itigi na manispaa ya Singida.
Katika kipindi cha Januari hadi Machi 2019, Jumla ya huduma za mkoba 747 zilipangwa kufanyika kwenye maeneo ambayo hakuna vituo vya kutolea huduma. Kati ya hizo ,ni huduma 534 tu zilizofanyika kutokana na changamoto za usafiri , hali mbaya ya hewa , uhaba wa watumishi na muingiliano wa kazi nyingine.
Mkoa unaendelea kusimamia Halmashauri kuhakikisha kuwa huduma za mkoba zinafanyika kama zinavyopangwa kwenye jamii hizi ili kutoa usawa wa upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto ikiwemo chanjo.
Katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2018 jumla ya watoto 6,6054 walifika kupata chanjo ya kwanza inayojulikana kama Pentavalent. Kati ya watoto hawa, ni watoto 61,021 walifika kukamilisha chanjo. Hii inamaanisha kuwa watoto 5,033 hawakufika kukamilisha dozi ya 3 ya chanjo hii muhimu inayokinga magonjwa mengi na hatari kwa pamoja kama homa ya ini, pepopunda, kifaduro, dondakoo na mafua makali.
Katika kipindi cha Januari hadi Machi, Jumla ya watoto 18,566 wamefika kupata dozi ya kwanza ya chanjo ya Pentavalent, kati ya hao watoto 16,722 wamefika kukamilisha dozi ya 3. Hii inamaana kuwa watoto 1,844 bado hawajafika kukamilisha dozi ya 3 itakayowapa kinga ya kudumu.
Aidha kipindi cha Januari 2018 hadi Machi 2019, Jumla ya watoto 6,877 walishindwa kufika ili kukamilisha chanjo hiyo muhimu. Kiasi hicho cha uasi kinaonekana katika chanjo nyingine zote zilizosalia.
Watoto kama hawa wanaoasi chanjo na wale ambao hawajafika kabisa kupata chanjo ndiyo wanaolengwa katika wiki hii ya chanjo ili waweze kupata kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali yanayozuilika kabisa kupitia huduma za chanjo.
Watoto wameendelea kuzaliwa nje ya vituo vya kutolea huduma hali inayosababisha kukosa baadhi ya huduma za awali za chanjo. Mkoa unasisitiza kuwa uzazi salama uzingatiwe, wazazi wajiandae na kufuata ushauri unaotolewa kliniki wakati wakiwa wajawazito ili kuwa katika mikono salama wakati wa kujifungua.
Hata hivyo, watoto wote wanapaswa kufikishwa kwenye vituo vya kutolea huduma ndani ya siku 14 za kuzaliwa ili wapatiwe chanjo hizo bila kujali wamezaliwa nyumbani au kwenye vituo vya kutolea huduma.
Hata hivyo watoto wote wanapaswa kufikishwa kwenye vituo vya kutolea huduma ndani ya siku 14 za kuzaliwa ili wapatiwe chanjo hizo, bila kujali wamezaliwa nyumbani au kwenye vituo vya kutolea huduma.
Mwaka 2018, serikali iliamua kuanzia chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake wote nchini kwa kuanza kuwachanja wasichana wenye umri wa miaka 14 kwanza.
Chanjo hii ilipokelewa vizuri hapo awali, lakini mwitikio ulipungua hasa kutokana na kupunguza kwa hamsa, Elimu na juhudi za kuwatafuta kuwachanja walengwa wa chanjo hii
Hadi kufikia Disemba 2018, Jumla ya wasichana 11, 352 walifikiwa kati ya walengwa 20,197 sawa na asilimia 56 tu.
Pia katika kipindi cha Januari hadi Machi 2019, Jumla ya wasichana 4,542 sawa na asilimia 82 wamefikiwa kupata dozi ya kwanza.
Takwmimu hizi zipo chini kwa lengo la mkoa ni kuwafikia wasichan wote wenye umri wa miaka 14.
Ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi huwapata wanawake kutokana na maumbile yao ya ndani kwani wanaume hawana kiungo hicho. Hivyo basi, licha ya ukweli kuwa vijidudu vinavyosababisha saratani ya mlango wa kizazi vinaweza kuwapata wanaume pia kwakuwa vinaenezwa kwa njia ya kujamiana, madhara yanayowapata wanawake ni makubwa mno hivyo hayawezi kufumbiwa macho.
Saratani ya mlango wa kizazi ipo na inawakumba wanawake wengi nchini
Katika mkoa wa Singida, Jumla wa wanawake 6, 018 walijitokeza kupata uchunguzi mwaka 2018. Kati ya hao, wmawake 385 walionekana kuwa na dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi
Pia katika kipindi cha Januari hadi Machi 2019, Jumla ya wanawake 1,956 wamejotokeza kufanyiwa uchunguzi, kati ya hao 17 wamegundulika kuwa na dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi. Dalili hizi za awali zinaweza kutibika na kupona kabisa iwapo mgonjwa atawahi matibabu.
Hata hivyo, siyo wanawake wote wanaogundulika kuwa na dalili hizi za awali wanafuata maelekezo na kurejea kupata matibabu ambayo ni muhimu sana ili kuzuia ugonjwa kuenea.
Nichukue nafasi hii kuwakumbusha wananwake wote ambao hawawezi kufikiwa na chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kuwa, kufika kupata uchunguzi na matibabu ni njia pekee ya kuzuia ugonjwa huu kabla haujaleta madhara makubwa mwilini. Ugonjwa ukiachwa uenee inakuwa vigumu kutibiwa na kupona.
Nitoe rai kwa jamii pia kuhakikisha mabinti zetu wanapata kinga kamili kwa kumalizia sindano zote 2 ili wasipate hizi changamoto ambazo wanawake wengi wanakumbana nazo na wengine kupoteza maisha.
Hata hivyo, chanjo hii haizuii magonjwa mengine kam virusi vya ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa, mimba za utotoni na madhara yote yanayotokana na kuanza ngono katika umri mdogo. Hivyo maadili na tahadhali ziendelee kuzingatiwa kwa ajili ya usalama wao dhidi ya hatari hizi nyingine
Udhibiti wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ni makubwa sana katika mkoa wetu na taifa kwa ujumla. Mgonjwa wa mwisho kuugua ugonjwa wa polio nchini Tanzania ilikuwa mwaka 1996.mgonjwa huyu aligundulika huko katika mkoa wa mtwara
Hata hivyo mafanikio haya yawe chachu kwetu kuongeza juhudi katika kutumia huduma za chanjo kwani kweli zinafanya kazi. Chanjo hutoa kinga kwa wale tu wanaopata huduma na kukamilisha ratiba.
Katika mkoa wetu wa Singida, Jumla ya wagonjwa 8 waligundulika kuugua ugonjwa wa surua mwaka 2015. Na mwaka unaofuata yaani mwaka 2016 wagonjwa wawili waligundulika kuugua ugonjwa huu hatari.
Hakuna wagonjwa wengine waliogundulika kuugua ugomjwa wa surua katika kipindi cha mwaka 2017 mpaka sasa, licha ya sampuli nyingi kuendelea kuchukuliwa kwa ajili ya uchunguzi kwenye maabara ya taifa.
Hata hivyo idadi ya watoto wasiokamilisha chanjo inaendelea kujitokeza kila mwaka, limbikizo hili linauweka mkoa wetu katika hatari ya kutokea mlipuko wa ugonjwa wa surua hivyo jamii ichukue tahadhali kwa kuhakikisha watoto ambao hawajakamilisha chanjo hii wanapatiwa huduma.
Katika upande mwingine, siku ya malaria duniani huazimishwa kila mwaka Tarehe 25.04. ni kawaida ya mkoa wetu kuadhimisha wiki ya chanjo sambamba na siku ya malaria duniani kwa kuwa mpaka sasa ugonjwa wa malaria hauna chanjo inayotolewa katika nchi yetu. Hivyo ninakuomba uwakumbushe wananchi juu ya ugonjwa huu hatari. Upo na bado unaua.
Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha malaria katika mkoa wetu ni aslimia 2.3 ingawa kiwango hiki ni chini ya wastani wa taifa ambao ni asilimia 7.3. bado kama mkoa tusijisahau, mapambano ni lazima yaendelee. Tunahitaji kufikia hatua ambayo hakuna mwananchi anayeugua ugonjwa huu.
Ili kukubali ugonjwa wa malaria, jamii inapaswa kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kuondoa mazalia ya mbu na kutumia vyandarua kwa usahihi.
Sambamba na hilo, serikali yetu inaendelea kuwakinga watoto kwa kuwaptia vyandarua bure kila wanapotimiza umri wa miezi 9. Vyandarua hivi hutolewa mtoto anapofikishwa kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua na rubella maarufu kama chanjo ya MR
Akina mama wajawazito pia kupatiwa vyandarua hivi bure kila wanapofika katika hudhurio la kwanza kwa ajili ya kumlinda mama na mtoto wake aliyetumboni
Katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2018, Jumla ya vyandarua 53,137 vimegawiwa kwa akina mama wajawazito sawa na asilimia 72.9. Pia vyandarua 42,650 vimetolewa kwa watoto sawa na asilimia 68.1
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.