Wajumbe wa Kikao cha Ushauri cha wilayani Iramba.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mhe: Simon Tyosela akichangia maoni yake kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya wilaya ya Iramba.
Mkuu wa wilaya ya iramba mkoani Singida Mhe: Emmanuel Luhahula amekuatana na kamati ya ushauri ya wilaya ya Iramba (DCC) leo tarehe 25 June 2019.
Kikao hicho kimeudhuliwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mhe: Simon Tyosela, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni, Waheshimiwa Madiwani na wadau mbalimbali wa maendeleo wa halmashauri ya wilaya ya Iramba.
Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa kikao ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe: Emamanuel Luhahula amesema wadau wote mnakaribishwa kushauri, kukosoa na kuchangia taarifa ya mada kuu ya uanzishwaji wa shamba la serikali kuu la miti ya migunga itoayo gundi katika uwanda wa mbuga ya wembere katika wilaya ya Iramba
Akizungumza na Wadau wa kikao hicho Mhe: Luhahula alisema “Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umejipanga kuanzisha shamba kubwa la mfano kwa nchi nzima la miti ya Gundi kwenye Mkoa wetu ili kuinua uzalishaji wa gundi kwa faida ya jamii na nchi kwa ujumla. Aidha ikumbukwe kuwa Mkoa wa Singida hauna shamba la miti la Serikali Kuu,hii itakuwa ni fursa ya kipekee itakayotoa ajira kwa akina mama na vijana. Shamba hili litarudisha uoto wa asili na viumbe hai waliohatarini kutoweka.
Akitoa ufafanuzi kuhuhu uanzishwaji wa shamba la serikali kuu la miti ya migunga itoayo gundi katika uwanda wa mbuga ya wembere katika wilaya ya Iramba, Meneja Misitu Wilaya Iramba Ndg Shaban J. Nyamasagara lisema “Mbuga ya Wembere katika Mkoa wa Singida ipo katika Wilaya za Iramba na Ikungi. Katika Wilaya ya Iramba vipo jumla ya vijiji 15 vijiji vinavyopitiwa na Mbuga hii ya Wembere ambavyo ni Doromoni Mingela, Nsunsu, Migilango, Tulya, Luono, Nkonkilangi, Mgongo ,Kisonga-Shelui, Mseko, Msai, Ujungu,Masimba Mlandala na Ndurumo.
Mbuga hii inaanzia kwenye miinuko ya ardhi nyuzi 06, kusini mashariki ya Mkoa wa Tabora na Kusini Magharibi ya Mkoa wa Singida. Bonde la mbuga hii linaunda maingiliano ya ndani ya maji na Ziwa Eyasi kwa Mkoa wa Arusha. Mbuga ya Wembere imezalisha uoto wa Asili wa nyasi na miti mbali mbali ikiwemo miti aina ya migunga inayozalisha gundi ambayo inakadiriwa kuwa na eneo lipatalo hekta 160,000, ikijumuisha na Wilaya za Igunga, Kishapu na Meatu katika Mikoa ya Jirani ya Tabora,Shinyanga na Simiyu.
Miti inayozalisha gundi kwa wingi ni aina za Migunga ,kitaalamu inajulikana kama Acacia Senegal ambayo huzalisha asilimia 95 ya gundi yote na Acacia seyal,Acacia drepanolobium na aina ziingine kwa asilimia 5. Gundi hii duniani inajulikana kama ‘dhahabu ya jangwani’.
Viumbe wengine katika mbuga ya wembere
Kwa mujibu wa shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uhifadhi wa ndege wa porini, ni kuwa mbuga hii ni makao mazuri ya aina tofauti 177 za ndege wa porini. Shirika hili limeainisha aina nne za ndege waliohatarini kutoweka wanaoishi kwenye mbuga hii ambazo ni,
Maana ya gundi
Ni utomvu unaotoka kiasilia kwenye miti ya migunga aina ya Acacia senegal na aina ziingine za jamii ya migunga hasa wakati wa hali ya ukame na jua kali baada ya mvua kuacha kunyesha, Mti huu utoao gundi (Acacia Senegal) kwa lugha za wenyeji wa Iramba unaitwa mdulungu ambao hukua kwa urefu wa mita 5- 13
Namna ya kuzalisha miche ya miti ya gundi
Miti hii yaweza kuzalishwa kwa kutumia mbegu. Mbegu hizi zinakuwa salama zikivunwa kabla kasha mbegu (Pod) haijakauka ambapo mbegu husiwa kwenye kitalu kabla ya kupandikizwa kwenye shamba. Aidha unaweza kupanda kwa kutumia pingili kwa baadhi ya miti. Hivyo shamba halisi miche hupandwa kwa nafasi za mita 4 x 4, vilevile kwa kilimo mseto ni mita 10 x 10
Uvunaji wa gundi
Asilimia 95 ya gundi inayotoka kwenye mbuga ya Wembere huvunwa kwenye miti ya migunga inayoitwa kitaalamu Acacia Senegal na asilimia 5 iliyobaki huvunwa kwenye jamii ziingine za migunga.
Ulinganifu wa uzalishaji gundi duniani
Wazalishaji wakubwa wa Gundi ni Sudani Tani 50,000, Ethiopia Tani 28,000 na Nigeria Tani 17,000 kwa mwaka, wakati huo huo Tanzania tukizalisha tani 1,000 kwa mwaka.
Masoko ya gundi
Gundi ya Tanzania husafirishwa na kuuzwa kwenye nchi za Pakistan, India, Saudi Arabia, Uingereza na Ufaransa pia Makampuni yanayojihusisha na ununuzi wa gundi Tanzania ni pamoja na Mohamed Enterprises, Fida Hussein na Export Trading.
Ushuru wa gundi kwa miaka mitano iliyopita –singida
|
|
|
MWAKA
|
KILO ZILIZOVUNWA
|
THAMANI(TSH)
|
2013
|
40000
|
20,000,000
|
2014
|
50000
|
25,000,000
|
2015
|
30000
|
15,000,000
|
2016
|
40000
|
28,000,000
|
2017
|
42000
|
29,400,000
|
2018
|
26000
|
18,200,000
|
JUMLA
|
|
135,600,000
|
Dhamira ya tfs kuanzisha shamba la miti ya gundi -singida
Faida za gundi kwenye viwanda vya chakula
Faida za gundi kwenye madawa
Matumizi ya wenyeji.
Vikwazo vya uzalishaji gundi
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.