• Malalamiko |
    • Kuhusu sisi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Maoni |
Iramba District Council
Iramba District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

Sara Kitainda ametoa msaada wa vitanda 21 na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula kusaidia huduma za Afya Hospitalini Wilayani hapa.

Posted on: September 17th, 2020

Hemedi Munga, Irambadc

ded.irambadc@singida.go.tz

Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Emmanuel Luhahula amewataka wawekezaji wazawa waliopo kwenye taasisi mbalimbali na wadau wengine wanaowekeza kufuata taratibu za Nchi za uwekezaji.

Mkuu huyo wa Wilaya  ametoa wito huo juzi wakati akipokea msaada wa vitanda 21  toka Shirika la Sadeline Health Care lenye makao makuu yake Jijini Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika nje ya jengo la Halmashauri hiyo mjini hapa.

“Mkurugenzi wa Sadeline, Sara Kitainda nakushukuru sana kwa msaada huu, nina uhakika kuwa vitanda hivi vitawasaadia akina mama sehemu ya kulala ili wajifungue vizuri katika Hospitali yetu” ameshukuru na kuongeza kuwa

“Lazima turudishe shukrani kwenu maana kitendo hichi kinatufariji sana, na tunatoa wito kwa wasomi wote walioko kwenye taasisi mbalimbali kuendelea kuiunga mkono Wilaya yetu kwa kujitolea misaada mbalimbali”

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanavitunza vizuri vitanda hivyo ili viweze kuihudumia jamii kwa muda mrefu.

“Niombe Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha mnavitunza vizuri vitanda hivi ili vifanye kazi iliyokusudiwa kwa sababu leo hii sisi tupo kesho hatupo na tunatamani wanaokuja waendelee kufaidika na matunda ya vitanda hivi,” amesisitiza Luhahula

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sadeline Health Care, Sara Kitainda amesema kuwa vitanda hivi vimetoka katika Shirika la Rotary Club toka nchini Canada ambavyo vimegharimu takribani tsh 32.3milioni.

“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya, leo hii nimefarijika sana kukukabidhi vitanda 21 kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za Afya katika Hospitali yetu ya Kiomboi ili akina mama waweze kujifungua wakiwa mahali salama,” amesema Kitainda

Hata hivyo Kitainda ameongeza kuwa lengo la taasisi yao ni kusogeza huduma katika Wilaya hii hivi karibuni kwa kuanzisha tawi la taasisi hiyo.

 “Natoa wito kwa wadau mbalimbali kuungana nasi katika jitihada za kutoa huduma mbalimbali katika wilaya yetu. Taasisi yetu inatarajia kufanya kampeni ya kuhamasisha wananchi kupima tezi dume kwa njia ya kisasa pamoja na kupima shinikizo la damu bure.”

Halikadhalika, Sara ametoa wito kwa wataalam mbalimbali wa afya ikiwemo waliokwisha staafu hususan walioko nje ya Nchi na ndani ya Nchi ambao ni wazaliwa wa Wilaya hii kutoa ushirikiano wa dhati  kusaidia Wilaya hii kwa shughuli mbalimbali za maendeleo.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt Adam Mashenene ameishukuru taasisi hiyo ya Sadeline Haelth Care na kuahidi kutoa ushirikano pindi taasisi hiyo itakapoka fungua tawi lake Wilayani Iramba.

Hata hivyo Dkt Mashenene ameahidi kuvitunza vitanda hivyo kwa manufaa ya jamii kwa ujumla ili viweze kutoa huduma kwa muda mrefu.

Taasisi ya Sadeline Health Care yenye makao yake Makuu jijini Dar es Salaam imekuwa na utaratibu wa kuchangia vifaa vya huduma za Afya ambapo mwaka juzi ilitoa vitanda 18 na hivi karibuni Taasisi hiyo inatarajia kutoa mashuka Wilayani hapa.

MWISHO

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula akikagua vitanda vilivyo tolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sadeline Health Care, Sara Kitainda. Picha na Hemedi Munga

Vitanda mbalimbali vya kisasa vilivyotolewa  na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sadeline Health Care, Sara Kitainda ili kusaidia huduma za Afya Wilayani Iramba. Picha na Hemedi Munga

Tangazo

  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 - HALMASHAURI WILAYA IRAMBA December 22, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2018 HALMASHAURI YA WILAYA IRAMBA January 05, 2019
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2018 January 05, 2019
  • TANGAZO LA KULIPA KODI YA ARDHI. February 26, 2018
  • Angalia Zaidi

Habari mpya

  • Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala yatembelea na kukagua miradi ya maendeleo yenye Tsh 1.6 bilioni Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.

    January 21, 2021
  • Mkuu wa Mkoa wa Singida DKt, Rehema Nchimbi amewaagiza Makamanda wa TAKUKURU kuwafuatilia Wanasheria na Mahakimu wanowaumiza wananchi

    January 23, 2021
  • Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula agawa zawadi kwa wanafunzi 10 waliofaulu vizuri katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2020.

    January 08, 2021
  • Sara Kitainda ametoa msaada wa vitanda 21 na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula kusaidia huduma za Afya Hospitalini Wilayani hapa.

    September 17, 2020
  • Angalia Zaidi

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
Video Zaidi

Linki za Haraka

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Linki Zinazohusiana

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Kuhusu sisi

    KIOMBOI, IRAMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Simu: 026 - 2532253

    Simu: 026 - 2533001

    Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • FAQ
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.